http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

#VIDEO: Dereva wa Lissu Matatani aamriwa asakwe.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amemtaka dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu, ajitokeze ili awe...




Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amemtaka dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu, ajitokeze ili aweze kutoa maelezo yake kuhusiana na tukio la kupigwa risasikwa bosi wake.

Kamanda huyo amesema kwamba sababu ya kumtafuta dereva huyo aliyemtaja kwa jina moja la Adam ni kwa sababu alikuwa pamoja na majeruhi wakati tukio hilo linatokea lakini tangu kutokwea kwa tukio hilo dereva huyo hajaonekana.

"Tangu kutokea kwa tukio dereva hakuonekana. Lakini kupitia gazeti tumeona ameanza kufanya mahojiano jana. Sasa amewezaje kufika Dar es salaam na Dodoma asifike. Sababu za kutoonekana hazifahamiki. Dereva huyo ni mtu muhimu kwetu katika kutoa ushahidi. Natoa 'notice' afike ofisi ya Mkurugenzi wa makosa ya jinai Dar au ofisi ya Mkuu wa makosa ya jinai Dodoma atupe taarifa zinazohusiana na tukio hili. Tunaamini anazo siri za tukio hilo.

Kamanda Muroto ameongeza kuwa "Sheria yetu inasema mtu aliye na taarifa akashindwa kuzitoa kwa jeshi la polisi atakuwa amefanya mako. Na kwa nini asitoe.

Pia Kamanda huyo alimtaka Katibu Mkuu wa Chadema Dkt. Vicent Mashinji kufika kwa RCO mjini Dar es Salaam ama Dodoma kutokana kauli yake kuwa katika uchunguzi wao wamewabaini wahusika.

Amemtaka kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kwa sababu kuonekana kwenye magazeti haitoshi bali kushirikiana kama mwananchi ndiyo njia sahihi ya kuwabaini wahalifu.

Pamoja na hayo Kamanda Muroto ameongeza kuwa "Tukio hili lisichukuliwe kama mtaji wa kisiasa. Nimesikia chama fulani kinahamasisha watu kutoa damu. Nawaomba watulie watuachie polisi nafasi ya kufanya kazi yetu. Matokeo mengi yameshatokea ikiwepo mauaji ya Kibiti, Mauaji ya Askari wetu lakini jeshi la polisi lilifanya uchunguzi na kubaini".

Kamanda Muroto amesema Polisi Mkoani Dodoma wamekamata magari nane aina ya Nissan Patrol kwa ajili ya uchunguzi wa tukio la kupigwa kwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema)Tundu Lissu.

Kamanda Muroto amesema uchunguzi huo unafanywa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA).

"Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa wahalifu walikuwa na silaha ya SMG/SAR kutokana na maganda ya risasi yaliyokutwa eneo," amesema

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : #VIDEO: Dereva wa Lissu Matatani aamriwa asakwe.
#VIDEO: Dereva wa Lissu Matatani aamriwa asakwe.
http://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2017/09/09/Lissu_3.jpg?itok=Z3OGAx7n×tamp=1504969611
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/09/video-dereva-wa-lissu-matatani-aamriwa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/09/video-dereva-wa-lissu-matatani-aamriwa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy