http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Polisi yatoa ufafanuzi wa mabomu yaliyoua Arusha

Kamanda wa polisi Arusha Charles Mkumbo amewataka viongozi waliopo karibu na kambi za mazoezi ya kijeshi kuweka utaratibu wa kuwakumbus...





Kamanda wa polisi Arusha Charles Mkumbo amewataka viongozi waliopo karibu na kambi za mazoezi ya kijeshi kuweka utaratibu wa kuwakumbusha wananchi kutoa taarifa pindi wanapoona vitu wasivyovijua hasa vyenye asili ya chuma ili kuepusha madhara.

Kamanda Mkumbo ametoa hadhari hiyo alipokuwa akizungumzia tukio la vifo vya watoto watatu wakazi wa kata ya Loksale wilayani Monduli vilivyosababishwa na mlipuko wa bomu waliookota wakati wanachunga mifugo na kuanza kulichezea kama mpira ambalo lililipuka na kuwajeruhi vibaya miguuni.

Akizungumza kwa njia ya simu kamanda Mkumbo amesema licha ya kuwa tukio hilo ni la bahati mbaya lakini lingeweza kuepukika kama watoto hao wangeweza kutoa taarifa ya kitu walichokiona.

Kamanda Mkumbo amesema kuwa watoto hao wangeweza kufanya hivyo kama wangekuwa wanakumbushwa na wazazi wao mara kwa mara wanapokwenda machungani.

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Monduli Bw. Iddy Kimanta aliyezungumza na ITV kwa njia ya Simu amesema watoto hao wote ni wanafunzi wa shule ya msingi Nafko na wawili akiwemo Landisi Setabau miaka 12 na Samweli Nyandusi miaka 9 walikuwa wanasoma darasa la kwanza wakati mwingine aliyetajwa kwa jina la Seuri Losila miaka alikuwa darasa la tatu.

Viongozi wa eneo lililopotokea tukio hilo wamesema kimsingi tukio hilo ni bahati mbaya kwani kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakielimishwa juu ya kufuata maelekezo na mara nyingi wamekuwa wakitoa ushirikiano ikiwa ni pamoja kutoa taarifa wanapoona mabaki ya vyuma.

Kwa mujibu wa viongozi hao katika maeneo mengi ya wafugaji wakati wa likizo watoto huwasaidia wazazi wao kuchunga mifugo na pia wakati wote wamekuwa wakitoa taarifa wanapokutana na vitu kama hivyo na wahusika wamekuwa wakifika mara moja na kuvichukua.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Polisi yatoa ufafanuzi wa mabomu yaliyoua Arusha
Polisi yatoa ufafanuzi wa mabomu yaliyoua Arusha
http://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2017/09/17/mkumbo.jpg?itok=lRg-yCEm×tamp=1505668209
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/09/polisi-yatoa-ufafanuzi-wa-mabomu.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/09/polisi-yatoa-ufafanuzi-wa-mabomu.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy