Dkt. Harrison Mwakyembe. WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amepiga marufuku uandaaji na uendeshwaji wa mash...
Dkt. Harrison Mwakyembe.
WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amepiga marufuku uandaaji na uendeshwaji wa mashindano ya urembo (Miss Tanzania) na tuzo za muziki hapa nchini kutokana na ubabaishaji wa waandaaji wa mashindano hayo.
Mwakyembe amesema mashindano ya Miss
Tanzania yamegubikwa na ubabaishaji wa hali ya juu ambapo kwenye utoaji
wa tuzo kumekuwa na tabia ya kuchelewa kuwapa washindi zawadi
wanazoahidiwa jambo linaloleta usumbufu na mitafaruku.
Ameongeza kuwa watakaotaka kuandaa
mashindano hayo ni lazima zawadi wanazoahidi kuwapa washindi zipelekwe
ofisini kwa waziri huyo.
”Kwa sasa tutanakaa chini na
wadau wa burudani juu ya mashindano hayo, lakini tunataka tuzo ziwe na
(guaranteed sustainability) muendelezo wa uhakika na sio kufanyika kwa
kubahatisha tu!”, alisema Mwakyembe.
Kwa mara ya mwisho mashindano ya za
Miss Tanzania yalifanyika mwaka 2016 ambapo ilichukua takribani miezi 6
kwa Kamati ya shindano la Urembo la Miss Tanzania kumpatia mshindi zawadi yake.
Kwenye tuzo za muziki waziri
Mwakyembe amesema tuzo hizo zinahitaji marekebisho kwani zilikuwa
zikitegemea watu wachache kiasi kwamba wakinuna basi hakuna tuzo.




