Mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias maarufu Mc Pilipili amepata ajali mkoani Shinyanga wakati akimkwepa mwendesha baiskeli kati...

Mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias maarufu Mc Pilipili amepata ajali mkoani Shinyanga wakati akimkwepa mwendesha baiskeli katika Kijiji cha Bubiki, Kata ya Mondo mkoani humo na alikuwa na abiria mmoja ambaye naye amepata majeraha.
Ofisa uhusiano wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Mwanza , Lucy Joseph amethibitisha kupokewa Mc Pilipili na amesema taarifa zaidi kuhusu hali yake zitatolewa baadaye.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Katibu Muhtasi wa Kampuni ya Pilipili Events, Stella Maswenga amesema Mc Pilipili alialikwa mkoani Shinyanga kwa ajili ya kusherehesha harusi wikiendi iliyopita na alikuwa akisafiri kuelekea Mwanza.



