http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

BREAKING: Serikali imesema iko tayari kugharamia matibabu ya Lissu

Serikali imesema ipo tayari kugharamia matibabu ya Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu A...

Serikali imesema ipo tayari kugharamia matibabu ya Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu ambaye kwa sasa hivi yupo Jijini Nairobi kwa matibabu kufuatiwa shambulio alilolipata Septemba 7,mwaka huu Mkoani Dodoma.
Hayo yamesemwa Jijini Tanga na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Waziri Ummy Mwalimu alisisitiza Serikali inasubiri kupata maombi kutoka kwa familia ya mgonjwa ikiambatana na taarifa rasmi kutoka kwa madaktari kuhusu mahitaji ya matibabu zaidi ya mgonjwa”Serikali ipo tayari kugharamia matibabu zaidi ya Mhe.Lissu popote Duniani”. Akiwa kama Mtanzania na Mbunge,Serikali inayo wajibu wa kugharamia matibabu yake hadi apone ili aweze kuendelea na kazi ya kuwahudumia Watanzania na wana Singida Mashariki.
Serikali inapenda kusisitiza kwamba iko tayari kuendelea kushughulikia matibabu endapo maombi ya kufanya hivyo yatawasilishwa rasmi Serikalini,ikiwemo kupata taarifa ya maendeleo ya afya yake kutoka kwa Madaktari wanaomhudumia hapo Nairobi ambayo itatakiwa kupatikana kupitia ridhaa itakayotolewa na Mhe.Lissu au Mwanafamilia wa karibu kama taratibu za Kidaktari zinavyoelekeza.
Aidha, Serikali imeshangazwa na dhana ya kuchangishana kwa ajili ya matibabu ya Mhe. Lissu, kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kutokea matapeli watakaochangisha Watanzania fedha kwa madai kwamba Mbunge huyo amekosa hela za matibabu.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto anawashukuru Madaktari wa watoa huduma wote wa Hospitali ya Rufaa Dodoma kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya katika kuokoa maisha ya Mhe.Lissu na kumtakia apate nafuu haraka
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya
21/9/2017
Kama ulipitwa na Mbowe alivyoeleza Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : BREAKING: Serikali imesema iko tayari kugharamia matibabu ya Lissu
BREAKING: Serikali imesema iko tayari kugharamia matibabu ya Lissu
http://s3-us-west-2.amazonaws.com/millard-ayo-bucket/wp-content/uploads/2017/09/21162115/Screenshot_20170908-184704-660x4001.jpg
https://i.ytimg.com/vi/5Ro7uFzMgi0/default.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/09/breaking-serikali-imesema-iko-tayari.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/09/breaking-serikali-imesema-iko-tayari.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy