http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

TUNDU LISSU AIKWEPA TWEET ILIYOMPONDA DIAMOND NA KUNDI LAKE

Mwanasheria wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameikana akaunti ya Twitter iliyoandika maoni kumpongeza mwanamuziki Al...

Mwanasheria wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameikana akaunti ya Twitter iliyoandika maoni kumpongeza mwanamuziki Alikiba, huku ikiwa na picha ya wanamuziki wanaofanya kazi chini ya lebo wa Wasafi.


Lissu amesema hafahamu chochote kuhusu akaunti hiyo na maoni yaliyotolewa akitaka mwandishi amfafanulie.

“Wananisingizia kaka (mhariri wa Mwananchi), ni wimbo gani wa Alikiba?” akimaanisha haelewi chochote kinachoendelea kuhusu uwepo wa wimbo wa “Seduce Me.”

Amesema akaunti hiyo si yake: “Hiyo akaunti ya Twitter si yangu na nilishasema tangu mwaka jana kaka.”

Jana Agosti 29, akaunti hiyo ilikuwa gumzo kwenye mitandao ikiwa imebeba ujumbe unaosema: “Hakuna kitu kibaya kama wanaume sita kuvaa mawigi kupambana na mtu mmoja. #seduceme.



Tweet hiyo iliambatanishwa na picha ya Kundi la Wasafi wakiwa wamevaa mawigi ambayo waliitoa sambamba na wimbo wao wa “Zilipendwa”.

Mashabiki wanaomuunga mkono Alikiba walifurahi wakiamini kiongozi huyo amejiunga na wengine wengi ambao walijitokeza hadharani kumpongeza Alikiba.

Baadhi ya viongozi waliompongeza Alikiba ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla; Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete; Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja na Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Bulembo.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : TUNDU LISSU AIKWEPA TWEET ILIYOMPONDA DIAMOND NA KUNDI LAKE
TUNDU LISSU AIKWEPA TWEET ILIYOMPONDA DIAMOND NA KUNDI LAKE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiGEORSesqsP9qmDtVet_aXhQ-eL1TTa8SwKGqSlKmAlblKjEq11odmtaT4H8KrgFPb0_ccJMJRHxWai10U84zZBvy85JsFuHsDbXOKKAVqdNYsTlS1MkcOihm2HCi8sI1ugTB77jLAh4k/s640/IMG_20170830_175645.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiGEORSesqsP9qmDtVet_aXhQ-eL1TTa8SwKGqSlKmAlblKjEq11odmtaT4H8KrgFPb0_ccJMJRHxWai10U84zZBvy85JsFuHsDbXOKKAVqdNYsTlS1MkcOihm2HCi8sI1ugTB77jLAh4k/s72-c/IMG_20170830_175645.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/tundu-lissu-aikwepa-tweet-iliyomponda.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/tundu-lissu-aikwepa-tweet-iliyomponda.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy