http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Rais Paul Kagame ashinda uchaguzi kwa asilimia 98

Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda inasema kuwa Paul Kagame ameshinda uchaguzi wa uraisi uliyofanyika jana nchini humo. Tume hiyo imesema m...


Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda inasema kuwa Paul Kagame ameshinda uchaguzi wa uraisi uliyofanyika jana nchini humo.


Tume hiyo imesema matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais Kagame alishinda kwa asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa. Rais Kagame ambaye amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba sasa atahudumu muhula wa tatu wa miaka saba.


Wafuasi wake wanamsifu Kagame kwa kuleta utulivu na maendeleo ya kiuchumi nchini humo baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo maelfu ya watu waliuaawa.


Wapinzani wa bwana Kagame walikuwa ni Frank Habineza na Philippe Mpayimana

Rais Kagame aliingia madarakani mwaka 1994 wakati kundi lake la waasi lilichukua udhibiti wa mji mkuu Kigali na kukomesha mauaji ya kimbari ambapo watu 800,000 watusi na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa.


Katiba ya Rwanda ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2015 na kumpa Kagame fursa ya kusalia madarakani hadi mwaka 2034.


Wapinzani wa Kagame wamelalamika kuwa wafuasi wao wanahangaishwa, wakisema kuwa ndiyo imesababisha kuwepo watu wachache katika mikutano yao ya kabla ya kura. Hata hivyo chama tawala kimekana madai hayo.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Rais Paul Kagame ashinda uchaguzi kwa asilimia 98
Rais Paul Kagame ashinda uchaguzi kwa asilimia 98
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh5pDFKpwoZtEwcPvf5scz1kgW6-e1GXxLU_dKiTJLypytAvdwXUqnVRrCywjYSIQoSn8mo3uFAemoO0kJNFvubaRZmDX1ugdlOE8wsaFkl1we9rGp5E-x6q4eoozdC2u4DDWAbxLuj1Jd0/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh5pDFKpwoZtEwcPvf5scz1kgW6-e1GXxLU_dKiTJLypytAvdwXUqnVRrCywjYSIQoSn8mo3uFAemoO0kJNFvubaRZmDX1ugdlOE8wsaFkl1we9rGp5E-x6q4eoozdC2u4DDWAbxLuj1Jd0/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/rais-paul-kagame-ashinda-uchaguzi-kwa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/rais-paul-kagame-ashinda-uchaguzi-kwa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy