http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

RAIS MAGUFULI AIAGIZA JKT KUREJESHA ARDHI KWA WANANCHI

Rais John Magufuli ameagiza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kurejesha eneo la eka 50 walilopewa na Kijiji cha Mkata, baada ya kushindwa kuli...


Rais John Magufuli ameagiza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kurejesha eneo la eka 50 walilopewa na Kijiji cha Mkata, baada ya kushindwa kuliendeleza kwa miaka saba.

Rais ameagiza hatua hiyo ichukuliwe leo Alhamisi, Agosti 3 wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkata akiwa njiani kuelekea mkoani Tanga, ambapo alimwita Mkuu wa JKT wa eneo hilo na kumhoji kuhusu kuendeleza eneo hilo.

“Hili eneo tangu mmepewa ni miaka mingapi sasa? Mliomba ili mjenge muwekeze kwa kujenga kiwanda, lakini mmeshindwa sasa leo hii mrejeshe kwa wananchi ili waweze kumpa hata mwekezaji mwingine,”ameagiza Rais Magufuli na kushangiliwa na wananchi.

Amemweleza mkuu huyo wa JKT kwamba wakajenge kiwanda hicho kwenye kambi yao kwa kuwa wana eneo kubwa ambalo linatosha pia kwa uwekezaji huo.


Awali aliwataka wananchi hao kuwa na subira kuhusu ujenzi wa hospitali katika eneo hilo, kwa kuwa kuna shaka kwamba Sh500 milioni zilizotolewa kwa awamu ya kwanza zilitafunwa, hivyo kabla ya kuleta nyingine wanapaswa kujiridhisha na matumizi yaliyofanywa.


Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alipopewa nafasi ya kulitolea ufafanuzi jambo hilo amesema wanaunda kamati ambayo itachunguza matumizi ya fedha hizo ndipo waweze kuruhusu fedha zingine zipelekwe ili kuendeleza mradi huo.


Rais Magufuli yupo safarini ambapo Agosti 5 atakutana na Rais Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la Mradi wa bomba la kusafirisha mafuta Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : RAIS MAGUFULI AIAGIZA JKT KUREJESHA ARDHI KWA WANANCHI
RAIS MAGUFULI AIAGIZA JKT KUREJESHA ARDHI KWA WANANCHI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhlm3n2I_5-OtcN8gU874hwDkCOqsabjp6HKwALCidjgCTzdszNfw6SuSpu9EachaAl0ZsrqhdmTLVT03P3LkcBRPrW_th3KtsVMPbN-y_LcBlCqw3OMyt6R1O1jr6p05rdqi8OayCwz22m/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhlm3n2I_5-OtcN8gU874hwDkCOqsabjp6HKwALCidjgCTzdszNfw6SuSpu9EachaAl0ZsrqhdmTLVT03P3LkcBRPrW_th3KtsVMPbN-y_LcBlCqw3OMyt6R1O1jr6p05rdqi8OayCwz22m/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/rais-magufuli-aiagiza-jkt-kurejesha.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/rais-magufuli-aiagiza-jkt-kurejesha.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy