http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

RC Gambo ahoji uhalali wa nyumba za ibada uwanja wa nanenane Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amehoji uhalali wa nyumba za ibada kujengwa ndaniya Uwanja wa maonyesho Nanenane eneo la Njiro mkoani A...



Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amehoji uhalali wa nyumba za ibada kujengwa ndaniya Uwanja wa maonyesho Nanenane eneo la Njiro mkoani Arusha.

Mkuu wa mkoa huyo ameshangazwa pia kuona ndani ya mabanda hayo kuna watu wanaishi na kusema ipo sababu ya kuhoji uhalali wa watu hao kuishi ndani ya viwanja hivyo pamoja na makanisa yakiwa ndani ya eneo la mabanda ya maonyesho hayo.

Hata hivyo Gambo amelazimika kumuagiza Mkuu wa Wilaya ya Arusha kuchunguza ubadhirifu wa mali na fedha uliofanyika kwenye mabanda hayo maonesho ya Nanenane. Amesema maandalizi ya maonyesho ya nanenane yataandaliwa na ofisi yake kupitia kwa katibu tawala na si Chama cha Wakulima na Wafugaji Tanzania,(TASO) kama ilivyozoeleka. "Sababu za kukatazwa kushiriki maonyesho hayo kwa nchi nzima ni kutokana na utendaji kazi wao mbovu na ubadhilifu wa fedha, hivyo tunatekeleza agizo la serikali " Mpaka sasa maandalizi ya maonyesho ya Nanenane yanaendelea vizuri na tunategemea Makamu wa Rais mheshimiwa Samia Suluhu anategemewa kuzindua maonesho haya,"amesema Gambo

Mkuu wa mkoa wa Manyara John Bendera ,amesema maagizo ya kutoshiriki kwenye maandalizi ya maonyesho kwa TASO ni maagizo ya kiserikali kutokana na chama hicho kushindwa kutenda kazi zao. Amesema pamoja na agizo hilo,bado wako kwenye mikakati ya kukabidhiana majukumu na chama hicho na kuwataka wananchi wanaotaka kushiriki maonyesho hayo kwenda kulipia mabanda yao kwa katibu tawala wa mkoa Arusha na si TASO kama ilivyokuwa hapo awali.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : RC Gambo ahoji uhalali wa nyumba za ibada uwanja wa nanenane Arusha
RC Gambo ahoji uhalali wa nyumba za ibada uwanja wa nanenane Arusha
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiImxSQsW25RRR9RUeNvW_oPtq3GuAswdoVSRzd5XK7mJJwm-rOqUiUSHv71eJEUTPM3nx3Jl2z3c-yoYNAE7YztyaM1d0ixJCFLBj1aGAWlpCJExo2BgJj5M-275lVT6a0hljgpC8tLetz/w1200-h630-p-k-no-nu/%255BUNSET%255D
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiImxSQsW25RRR9RUeNvW_oPtq3GuAswdoVSRzd5XK7mJJwm-rOqUiUSHv71eJEUTPM3nx3Jl2z3c-yoYNAE7YztyaM1d0ixJCFLBj1aGAWlpCJExo2BgJj5M-275lVT6a0hljgpC8tLetz/s72-w1200-c-h630-p-k-no-nu/%255BUNSET%255D
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/07/rc-gambo-ahoji-uhalali-wa-nyumba-za.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/07/rc-gambo-ahoji-uhalali-wa-nyumba-za.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy