http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Jeshi la Polisi Laua Wahalifu Wawili Kibiti

Jeshi la Polisi nchini limewaua watu wawili wanaodaiwa kufanya mauaji katika Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji, mkoani Pwani. Akie...


Jeshi la Polisi nchini limewaua watu wawili wanaodaiwa kufanya mauaji katika Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji, mkoani Pwani.


Akielezea tukio hilo jana (Alhamisi Julai 6) , Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea Jumatano saa nne usiku katika msitu wa Ngomboroni Kata ya Ikwiriri, Wilaya ya Ikwiriri.


Wahalifu hao waliuawa na askari wa operesheni maalumu wakiwa katika doria za ufuatiliaji wahalifu sugu wanaojihusisha na mauaji yanayoendelea katika kanda hiyo ya kipolisi.


Alisema askari wakiwa na mtuhumiwa mmoja muhimu anayeshiriki katika mauaji hayo ambaye alikamatwa, alikubali kwenda kuwaonyesha polisi mahali ambapo ni maficho ya wenzake.


“Baada ya kufika eneo la msitu wa Ngomboroni kikundi cha watu wanaokadiriwa kufikia watano walikurupuka kutoka kwenye kichaka na kuanza kukimbia ndipo polisi kwa tahadhari kubwa walianzisha mashambulizi na kufanikiwa kumjeruhi mhalifu mmoja kwa risasi, katika mashambulizi hayo mtuhumiwa aliyekuwa mkononi mwa polisi naye alijaribu kutoroka na hivyo kupelekea kumjeruhi kwa risasi hivyo idadi yao kufikia wawili,” alisema.


Aliongeza; “majeruhi hao wawili walifariki dunia njiani wakati wakipelekwa hospitali kwa matibabu kutokana na kuvuja damu nyingi iliyosababishwa na majeraha ya risasi waliyoyapata. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.”


Kamishna Sabas alisema katika tukio hilo wamefanikiwa kupokonya silaha mbili aina ya SMG na Shotgun moja pamoja na risasi tisa.


Kamishina Sabas amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu wengine waliosalia na kwamba zawadi nono bado ipo pale pale na itatolewa kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa sahihi kuhusiana na wahalifu wanaojihusisha na mauaji katika kanda maalumu ya Rufiji.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Jeshi la Polisi Laua Wahalifu Wawili Kibiti
Jeshi la Polisi Laua Wahalifu Wawili Kibiti
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhaG-vGv5pLpmniq_VYWVA9d45HUECvSg2uM6EoTlkFsLH8O1eki1HUPCNwCzqJsjtNIf7w0DBTYn-FL0QTu4gmbhoLaHBwOO_wh6oyiwr8agbuvB1TE3dlOHRs6V6gAVLkz86aC44XR5d_/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhaG-vGv5pLpmniq_VYWVA9d45HUECvSg2uM6EoTlkFsLH8O1eki1HUPCNwCzqJsjtNIf7w0DBTYn-FL0QTu4gmbhoLaHBwOO_wh6oyiwr8agbuvB1TE3dlOHRs6V6gAVLkz86aC44XR5d_/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/07/jeshi-la-polisi-laua-wahalifu-wawili.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/07/jeshi-la-polisi-laua-wahalifu-wawili.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy