Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limeanza kuchukua hatua kali na kufuta leseni za pikipiki ambazo wamiliki wake wanaajiri madereva wasiyo n...
Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limeanza kuchukua hatua kali na kufuta leseni za pikipiki ambazo wamiliki wake wanaajiri madereva wasiyo na leseni ambao wanatajwa kuwa chanzo cha ongezeko la ajali pamoja na matukio ya kihalifu
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo ametoa kauli hiyo wakati maafisa wa jeshi la polisi walipokutana na wamiliki pamoja na madereva wa boda boda kujadili ongezeko la ajali na matukio ya kihalifu.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha Nuru Selemani amesema katika ajali zinazotokea kwa mwaka mkoa wa Arusha ajali za pikipiki ni zaidi ya nusu ya ajali hizo.
Mwenyekiti wa umoja wa waendenda wa boda boda mkoa wa Arusha Maulid Makongoro amesema wataendelea kutoa ushirikiano kubaini wanaofanya matukio ya kihalifu lakini wanaomba jeshi litunze siri kwa wanaopeleka taarifa hizo.



