Na Raymond William ONDOKANA NA AIBU YAKUANZIA CHINI. Msomaji na wewe uliye mdau wa Blog ya Wepesi Media nikushukuru sa...
Na Raymond William
ONDOKANA NA AIBU YAKUANZIA CHINI.
Msomaji na wewe uliye mdau wa Blog ya Wepesi Media nikushukuru sanaa kwa kutembelea Blog hii, Ndani ya Makala yetu ya AIBU NDANI YA AKILI Tuwe pamoja mwanzo mpaka tamati.
Mtu yeyote, anaweza kujijengea
mafanikio makubwa kabisa kwa kuanzia pale alipo sasa.
Hii ina maana kwamba kama huna pa kuanzia kabisa, basi unaweza kuanzia chini kabisa, ukawaka juhudi na maarifa, ukawa mvumilivu na king’ang’anizi na ukaweka muda na hatimaye ukafikia mafanikio makubwa. Ni kitu ambacho kinawezekana, lakini siyo rahisi.
Hii ina maana kwamba kama huna pa kuanzia kabisa, basi unaweza kuanzia chini kabisa, ukawaka juhudi na maarifa, ukawa mvumilivu na king’ang’anizi na ukaweka muda na hatimaye ukafikia mafanikio makubwa. Ni kitu ambacho kinawezekana, lakini siyo rahisi.
Na ugumu zaidi unaongezwa na mtazamo wa watu juu yetu, pale ambapo tunafikiria kwamba watu wengine watatuonaje pale wakituona tunafanya mambo ambayo yapo chini yetu. Labda tumesoma mpaka vyuo vikuu, na huna pa kuanzia, ukifikiria uanze biashara ndogo unaona watu watakudharau, na kukuona na elimu yako yote unafanya biashara kama hiyo! Kwa mtazamo huu wengi wanaona aibu, wanahofia na kuacha kabisa kufanya.
Mwishowe wanabaki pale walipo, maisha yanazidi kuwa magumu zaidi.
Leo kwenye makala yetu ya aibu ndani ya akili, tutakwenda kuangalia jinsi unavyoweza kuondokana na changamoto hii ya kuwa na aibu ya kuanzia chini kabisa.
Jamii imetufanya tuamini kwamba, kwa kuanza kidogo basi tu watu wa chini, watu tusiofaa na watu ambao hatutafika popote. tumepokea imani hiyo ya jamii kwa utiifu kabisa na kuchagua kuiishi.
Zingatia mambo yafuatayo ili kuondokana na aibu ya kuanzia chini.
1. Hakuna anayejali sana maisha yako zaidi yako mwenyewe.
Binadamu wote huwa tunafanya kosa moja kubwa sana, huwa tunaamini kama vile dunia nzima inatuangalia kwenye kila tunachofanya. Tunafikiri kwamba watu usiku wanakosa usingizi wakifikiria yale ambayo tunafanya au kutokufanya.
Ukweli ni kwamba watu wanafikiria zaidi maisha yao kuliko wanavyoyafikiria maisha yako. Watu usiku wanakosa usingizi kwa matatizo yao na siyo kuhusu wewe. Mtu anaweza kukuambia jambo la kukatisha tamaa, lakini usifikiri ndiyo atakufikiria wewe wakati wote, atarudi kufikiria matatizo yake.
Jipe uhuru wa kufanya kile ambacho unataka kufanya, kwa sababu kila mtu anahangaika na mambo yake. Hakuna atakayepoteza muda wake kukufuatilia wewe kwa kila unachofanya. Na atakayefanya hivyo basi jua yeye mwenyewe hana maisha ya maana kwake, na hivyo hana umuhimu wowote kwako.
.......................................................ITAENDELEA
Usikose Mwendelezo wa makala hii inayochapishwa ndani ya Blog ya wepesi media....tutembelee kila siku kujua nini kinaendelea.
MAWASILIANO
Phone: 0754954872
Email: prblessing94@gmail.com




