KARIBU KATIKA SIMULIZI YA KUVUTIA YA "THAMANI YANGU IKO WAPI" Mtunzi na Mwandishi; Khaji Juma Shaaban E-...
KARIBU KATIKA SIMULIZI YA KUVUTIA YA
"THAMANI YANGU IKO WAPI"
Mtunzi na Mwandishi;
Khaji Juma Shaaban
E-mail: khaji1juma@gmail.com
Phone no: +255 765 533 840
Kabla ya kusonga mbele na simulizi yetu napenda kuwakumbusha tuliishia wapi katika sehemu ya pili:
Specioza tayari alikuwa akiendelea na matibabu na Mzee Lucas ambaye ndiye Baba mzazi wa Specioza tayari alikuwa amekwishawasili Hospitalini hapo ili kujua hatima ya mwanaye, baada ya kuonana na daktari na kumuahidi kumpatia mali zake pindi atakaposaidia kuyaokoa maisha ya binti yake punde si punde Mzee Lucas alionana na jirani yake na wakawa katika mazungumzo mafupi kabla ya kusikika sauti za vilio vya nguvu zilizokuwa zikitokea eneo la wodi aliyokuwa amelazwa Specioza jambo lililomfanya Mzee Lucas kujikuta akipiga kelele kwa kuliita jina la Binti yake Speciozaaaaaaaaa……………
SEHEMU YA III.
Wagonjwa wote walihamaki baada ya kuisikia sauti hiyo iliyokuwa na simanzi kubwa ya mfano wa mtu aliyechomwa sindano kwenye kidonda kibichi na kujikuta wakiamka kutoka katika vitanda vyao kushuhudia ni wapi ilipokuwa ikitokea sauti hiyo na ilikuwa ni ya nani na kwanini alie kwa uchungu namna hio.
Sekunde kadhaa kitanda chenye magurudumu ambacho ni mahususi kwa kubebea wagonjwa mahututi kikaonekana kikisukumwa kutokea eneo lilelile la wodi aliyokuwa amefikishiwa mtoto Specioza na kulionekana kunamtu aliyekuwa amefunikwa mwili mzima kuashiria ameaga dunia.
Wahudumu waliokuwa wakikisukuma kitanda hicho walionekana wakiwa na haraka zaidi huku wakielekea sehemu ya kuhifadhia maiti (Mochwari) hawakutambua chochote kilichokuwa kikiendelea kwa wakati huo walipita karibu kabisa na mzee Lucas na jirani yake walipokuwa wamesimama wakati wanawapa mgongo ghafla upande mmoja wa shuka lililokuwa limefunika mwili huo likapgwa na upepo na kuachia upenyo kidogo,
Wakati wote huo mzee Lucas hakuweza hata kuruhusu hata kope ya jicho lake kufunga ndipo aliposhuhudia kupitia katika upenyo ule na kuuona mkono uliokuwa ukijieleza dhahiri kuwa ni mkono wa jinsia ya kike.
Hapo ndipo mzee Lucas alipopata ujasiri na kujikuta akikimbia mbio mithili ya mtu aliyeko katika mashindano ya marathoni huku akifuata kile kitanda.
Alifika na kumsukuma muuguzi mmoja na kuufunua mwili ule huku akisema maneno yaliyosikika kwa sauti ya malalamiko ikisema..
“Kwanini imekuwa mapema hivi kipenzi changu Specioza unaniacha na nani sasa mimi Baba yako rudi baasi tuendelee na maisha kama ilivokuwa mwananguu..”
Wauguzi na wagonjwa wengine walikuwa wamepigwa na butwaa wakimtazama mzee huyo aliyeshindwa kuzizuia hisia zake huku kila mgonjwa akisikika akizungumza na mwenzake kwa maneno ya chinichini wakisema
“Hii ndio njia ya wote huyo katangulia hatujui ni nani atakayefuata masikini bado alikuwa ni binti mdogo sana Mungu kamuwahisha kabla hata hajatimiza ndoto zake”.
Mzee Lucas alishindwa kujizuia na kujikuta akivuta lile shuka lililokuwa limeufunika mwili wa binti huyo ghafla alichokishuhudia kilimfanya akajikuta ametoa macho mithili ya mjusi aliyebanwa na mlango kwa kile alichokishuhudia,
Kichwa kilikuwa kimepasuka,mwili mzima umeharibika vibaya nguo zote zilikuwa zimejaa damu kwa mtu mwenye roho nyepesi asingeweza kuutazama mwili huo katika kuutazama mwili huo aliona sehemu ya mguu wa kushoto ilikuwa imefungwa karatasi iliyokuwa na jina la Marry.
Mzee Lucas akajikuta akikosa hata nguvu na alishindwa kujua kitu chakufanya na hapo ndipo alipoelezwa kuwa binti huyo amefikishwa hospitalini hapo akiwa tayari amekwishakupoteza maisha kutokana na ajali iliyohusisha gari na bodaboda na binti huyo alikuwa ni abiria wa bodaboda huyo.
Alijikuta akirudi kwa kasi tena alipokuwa amelazwa binti yake na kabla ya kufika alishuhudia kundi kubwa la wanafunzi likiwa karibu na mlango wa wodi hiyo hapo alihisi kupigwa na ubaridi ambao haukuelezeka kirahisi na kujikuta akisimama pasipo kuelezwa na mtu yeyote,
Wanafunzi hao walishindwa kumtambua kwa haraka mzee huyo alikuwa ni nani hasa ndipo walipoweza kufahamishwa na Mwalimu Robert ambaye walikuwa wameongozana naye kuja kumtembelea mwanafunzi mwenzao kuwa anaitwa Mzee Lucas ambaye ndiye Baba mzazi wa Specioza.
Kila mwanafunzi alijikuta akitoa sauti ya kumsalimia na kumpa pole kwa kilichotokea juu ya binti yake.
Wakati wote huo hapakuwa na taarifa yoyote iliyokuwa imetoka ndani ya wodi imuhusuyo Specioza mpaka majira ya saa kumi na mbili na nusu watu walitakiwa kuondoka kwani muda ulikuwa umekwisha wa kuona wagonjwa na Madaktari hawakuruhusu mtu yeyote kuingia wala kubaki katika wodi hiyo.
Mpaka majira ya saa tatu usiku Mzee Lucas alikuwa bado yupo maeneo ya wodi hiyo akihakikisha chochote kitakachotokea kwa binti yake aweze kukitambua kwani alikuwa yuko tayari kwa kitu chochote ambacho kingehitajika kuweza kuokoa maisha ya binti yake.
Kufikia majira ya saa nne usiku eneo la hospitali hio palitawala ukimya na baadhi ya wagonjwa walikuwa tayari wamepitiwa na isingizi huku wengine wakionekana kumeza dawa ili waweze kupumzika.
Upande wa pembeni ya wodi aliyokuwa amelazwa Specioza palionekana kijana mmoja aliyekuwa akifanania na wagonjwa waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo kulingana na muonekano wake alivyokuwa amechoka na kuchakaa huku mavazi yake yakionekana yameraruka mithili ya kichaa aliyetoka dampo.
Kila mmoja hakuwa na wazo lolote dhidi ya kijana huyo na kujikuta wakiendelea na shughuli kama kawaida.
Ghafla madaktari wakaonekana wakipishana mara kwa mara wodini hapo kuashiria hali isiyokuwa nzuri upande wa ndani na ndipo zikawa zinasikika sauti kutoka ndani ya wodi huku madaktari wakionekana wakiwa wameshikilia vifaa mkononi ambavyo vilidhihirika kuwa ni vifaa maalumu vya kushitulia mapigo ya moyo,
“Moja mbili tatu shtuaa!!!” ndizo sauti zilizokuwa zikisikika kupitia mlango uliokuwa umeachwa wazi kidigo
Mzee Lucas alisikika akimuomba Mungu kwa sauti ya huruma na upole…
“Eee Mwenyezi Mungu kama umeshindwa kuyasikia maombi yangu ya kumrudishia uhai binti yangu nakuomba basi umchukue tu taratibu apumzike ila usimzidishie mateso kama haya”.
Upande wa Madaktari waliendelea na juhudi hizo za kutaka kurudisha mapigo ya moyo ya mtoto Specioza jambo la tofauti likasikika kutokea nje ambapo hata Madaktari walijikuta wakistaajabu kwa kilichotokea mbele ya macho yao.
Sauti ya mvuto wa aina yake ilisikika kutoka nje ya wodi hiyo iliyokuwa imejaa nakshinakshi tele huku ikisikika ikitamka maneno hayaaa……..
“So here we stand in our secret place with a sound of the crowd so far away,
And you take my hand and it feels like home we both understand its where we belong,
So how do I say? Do I say goodbye we both have our dreams we both wanna fly,
So lets take tonight to carry us through the lonely times
I will always look back as I walk away this memory will last for eternity,
And all of our tears will be lost in the rain,
When I have found my way back to your arms again,
But until that day you know you are the queen of my heart………….”
Ghafla Madaktari walishangaa kuona Specioza akifungua macho huku akishusha pumzi ya jazba na hasira baada ya kuisikia sauti hiyo iliyokuwa ikiimba wimbo wa West life unaotambulika kwa jina la Queen of my heart…………..!!!!!!!!!!
Itaendelea………….
Usikose kufuatilia sehemu ya Nne itakayotoka siku ya kesho ili kujua nini kitaendelea.
Nawashukuru wale wote wanaoendelea kutoa ushauri kuhusu wapi tuboreshe na kipi kifanyike ili kuupata uhondo wote bila kukosa hata chembe ya uhondo. Endelea kufuatilia Simulizi hii na Mungu akubariki piaa.