Diwani wa kata ya Murriet halmashauri ya Jiji la Arusha kupitia (Chadema) Mhe Credo Kifukwe amejiuzulu nafasi yake ya udiwani kwa kile amb...

Diwani wa kata ya Murriet halmashauri ya Jiji la Arusha kupitia (Chadema) Mhe Credo Kifukwe amejiuzulu nafasi yake ya udiwani kwa kile ambacho amesema kuwa ni anaunga mkono Utendaji kazi wa raisi Magufuli.
"Ninajiuzulu nafasi yangu ili niweze kumuunga mkono Rais Magufuli katika utendaji wake,dhamira inanisuta kuwa katika kundi linalopinga kila kitu" alisema Mhe Credo.
Mheshimiwa Credo amenukuliwa akisema wakati wa kutoa tamko la kujiuzulu kwake kuwa "Ninajiuzulu nafasi yangu ili niweze kumuunga mkono Rais Magufuli katika utendaji wake, dhamira inanisuta kuwa katika kundi linalopinga kila kitu" alisema Mhe Credo.
Mhe Credo anakuwa ni Diwani wa 11 wa UPINZANI kujiuzulu tangu kuisha kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.



