http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Mwakyembe: Taarifa za uvamizi Clouds hazitoshi kwa mimi kutoa uamuzi wowote

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, jana baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam, amekiri kuwa ...


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, jana baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam, amekiri kuwa anafahamu kuhusu tukio la uvamizi lililofanyika katika ofisi za Clouds Media Group.


Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Mwakyembe aliyechukua nafasi ya aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye alisema kuwa yeye kwa sasa hawezi kulizungumzia tukio hilo wala kutoa uamuzi wowote kwa kuwa hajapata ushahidi unaojitegemea.


“Ninachokijua kuhusu hilo tukio kinatokana na taarifa za vyombo vya habari, taarifa za magazeti, za redio, za televisheni, na sidhani kama taarifa hizo zinatosha kwa mimi kutoa uamuzi wowote.”


Ameongeza kuwa bado suala hilo ni la kuchunguzwa zaidi kwani picha inayotolewa ni ya upande mmoja.


“Mlalamikaji hapa ni Clouds, anayetupa taarifa kuhusu suala hili zima ni Clouds na wenzake. Kwa hivyo naipata picha hii kwa upande mmoja…”


Aidha kwa mujibu wa ripoti iliyokuwa imetolewa na kamati iliyoundwa na aliyekuwa Waziri, Nape Nnauye ilisema kuwa wamesikiliza upande wa mlalamikaji (Clouds Media Group).


Lakini walipokwenda kwa ajili ya kuusikiliza upande wa mlalamikiwa (RC Paul Makonda) hawakufanikiwa kumpata.


Hii ni baada ya wao kusubirishwa kwa muda mrefu nje ya ofisi yake na baadae kuambiwa kuwa Makonda ameondoka na hatoweza kurudi kwa siku hiyo. Jambo hili liliwafanya wajumbe hao kujiaminisha kuwa Makonda hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo na aliamua kuwatoroka.


Hata hivyo ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa aliyekuwa Waziri, Nape Nnauye ili aifikishe katika mamlaka husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.

Credity.....Mpekuzi.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mwakyembe: Taarifa za uvamizi Clouds hazitoshi kwa mimi kutoa uamuzi wowote
Mwakyembe: Taarifa za uvamizi Clouds hazitoshi kwa mimi kutoa uamuzi wowote
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjc_CQomYWylP1WGYgxpJgr4qHSut42PAZweZ_U4Crcrd-M09lycBiTnNLRKUq1brmA82SkNqZv9mUoYJJmDvt7f95WwE2qt4uVpPrRBkcMU7F7y0BVJgg1xlZ2m5_OxZJRQGKVChNP0i0k/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjc_CQomYWylP1WGYgxpJgr4qHSut42PAZweZ_U4Crcrd-M09lycBiTnNLRKUq1brmA82SkNqZv9mUoYJJmDvt7f95WwE2qt4uVpPrRBkcMU7F7y0BVJgg1xlZ2m5_OxZJRQGKVChNP0i0k/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/mwakyembe-taarifa-za-uvamizi-clouds.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/mwakyembe-taarifa-za-uvamizi-clouds.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy