http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Lowassa Akawaribisha UKAWA Kina Sophia Simba Waliovuliwa Uanachama CCM

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amekaribisha waliokuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwamo aliyekuwa Mwenyekiti wa Umo...


Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amekaribisha waliokuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwamo aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT), Sophia Simba kujiunga na Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).


Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), aliyasema hayo jana katika taarifa yake.


Alisema wanachama hao walikuwa mashujaa wa kutetea haki, demokrasia na taratibu kwa kupinga dhuluma ndani ya chama chao cha CCM.


“Nafsi yangu imenisukuma kushika kalamu na kuandika haya kutokana na kile kilichotokea Dodoma katika vikao vya CCM.


“Ni takriban miezi 20 sasa toka nilipojitoa CCM, lakini nasikia bado naendelea kutajwatajwa huko katika vikao vyao.


“Wamewatimua wanachama na viongozi wao ambao wengi wao walitumia demokasia yao kupinga upindishwaji wa kanuni na sheria za chama chao.


“Nataka kuwaambia kuwa wakati wakifanya hivyo walikuwa mashujaa wa haki na demokrasia na misingi ya utawala bora nchini,” alisema Lowassa katika taarifa yake


Mjumbe huyo wa Kamati Kuu alisema wanachama hao wa CCM walisimamia kile walichokiamini bila ya kuvunja sheria, wamekata minyororo ya unyonge na uonevu.


“Mbegu ile waliyoipanda itamea na kuzaa matunda demokrasia ya kweli nchini kwetu.


“Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba upinzani wa kweli utatokea CCM, naamini usemi huo sasa unatimia kwa kasi kubwa.


“Nawakaribisha Chadema na Ukawa kwa jumla huku kuna maisha mazuri sana, hakuna minyororo ya utumwa wa siasa. Kilichowapata ni sawa na kumpiga chura teke unamuongezea kasi tu.


“…waje wajiunge nasi katika safari ya kuleta demokrasia ya kweli na siasa zenye ukomavu, safari hii inahitaji umoja na mshikamano kufikia malengo,” alisema.


Lowassa alisema anashangazwa na namna hatua ya CCM kujinasibu kuwa CCM ikiyumba.


Alisema nchi itayumba lakini anaamini kinachotokea na jinsi CCM inavyoyumba ndivyo wananchi wanavyozidi kukomaa katika siasa na kuimarika katika harakati za kutafuta mabadiliko ya kweli.


Alisema Watanzania wa sasa hawawezi tena kuvumilia ukandamizaji wa haki zao za msingi unaofanywa na watawala.


“Nidhamu ya woga haina tena nafasi katika kujenga nchi yenye kuheshimu misingi ya haki demokasia na utawala bora,” alisema.


Juzi, CCM kilitangaza kuwafukuza wanachama wake 12, akiwamo Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT), Sophia Simba, ambaye wiki iliyopita alitangaza kutogombea tena nafasi hiyo.


Wengine waliofukuzwa ni wenyeviti mikoa ambao ni Jesca Msambatavangu (Iringa), Erasto Kwilasa (Shinyanga), Ramadhan Madabiba (Dar es Salaam) na Christopher Sanya (Mara).


Waliofukuzwa wengine ni Willfred ole Mollel ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini, mjumbe wa NEC wa Wilaya ya Babati Mjini, Ally Sumaye na Mathias Manga wa Wilaya ya Arumeru.


Katika orodha hiyo pia wamo wenyeviti wa wilaya wa chama hicho ambao ni Omari Awadhi (Gairo), Ally Msuya (Babati Mjini), Makolo Laizer (Longido) na Salumu Madenge (Kinondoni-Dar es Salaam).


Wanachama wengine waliochukuliwa hatua baada ya kufanya makosa kama hayo kuwa ni Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi ambaye amepewa onyo kali na anatakiwa kuomba radhi.


Wakati Nchimbi akipewa onyo, Adam Kimbisa ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma na Mbunge wa Afrika Mashariki amesamehewa.


Kutokana na uamuzi huo Sophia atalazimika kupoteza ubunge. Ilielezwa kuwa amefukuzwa baada ya kupatikana na makosa ya maadili kinyume na Katiba na kanuni za chama hicho.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Lowassa Akawaribisha UKAWA Kina Sophia Simba Waliovuliwa Uanachama CCM
Lowassa Akawaribisha UKAWA Kina Sophia Simba Waliovuliwa Uanachama CCM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg2VEbjds_CMMVlOMnJveOqh-cCK8ivGeuCpPJ4Yz8ypYEe9aQKZjuTG_DSZ5kw7gzp8dEdZuxAnNegAcGYkjeF_ZkOMmrRhkRyHjvFbx_S6J61xDKcapUTY7wmAyRU9BWkSOEeOa1K_WFE/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg2VEbjds_CMMVlOMnJveOqh-cCK8ivGeuCpPJ4Yz8ypYEe9aQKZjuTG_DSZ5kw7gzp8dEdZuxAnNegAcGYkjeF_ZkOMmrRhkRyHjvFbx_S6J61xDKcapUTY7wmAyRU9BWkSOEeOa1K_WFE/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/lowassa-akawaribisha-ukawa-kina-sophia.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/lowassa-akawaribisha-ukawa-kina-sophia.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy