Na,Vero Ignatus ,Dar- es -salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Sirro amesema kuwa anausong...
Na,Vero Ignatus ,Dar- es -salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Sirro amesema kuwa anausongo na watu ambao watakaofanya fujo katika uwanja wa taifa watakaokwenda kutazama mechi kati ya simba na yanga ili awashughulikie kisawasawa
Ametoa rai hiyo alipokuwa akizungumza kwenye kituo cha East Africa Radio na kusema kuwa atakayekwenda kutazama mechi jumamosi ya tarehe 25 februari 2017 aingie salama na atoka salama bila kugusa kiti atakayekiuka sheria itafuata mkondo wake.
"Nasema hivi mama kama mwanao ni mtukutu bora umwambie asije uwanjani kabisa,mama kama mumeo ana mihemko anapotazama mechi na anatamani kuvuja viti bora abaki hukohuko asije uwa njani kabisa,kipindi kilichopita walivunja viti na waliniaibisha sana sasa safari hii sintakubali kuaibishwa tena"alisema Sirro.
Akizungumzia swala la kupambana na madawa ya kulevya Sirro amesema kuwa unaposikia watanzania wamekamatwa nje ya nchi ni aibu na uharibifu mkubwa ,inaharibu sifa ya nchi yetu hivyo lazima lishughulikiwe kwa kasi kubwa.
"Vita hii ya madawa ya kulevya oparesheni yake imekuwa kubwa imegusa watu wengi ambao walidhania hawatakamatwa,wamekamatwa,mwisho wa siku tumewakamata,tunawahoji,na wakikutwa na hatia tunawapeleka mahakamani, kama aliyekamatwa hajakutwa nayo anaachiwa kwani tatizo nini jamani"alisisitiza Sirro.
Akizungumzia changamoto mbalimbali za utendaji kazi amesema kuwa ni pamoja na askari kulalamikiwa huwa linamsumbua sana kwani askari ni kioo cha jamii,uhalifu ukizidi mahali haswa ukuzingatia jeshi la polisi na wananchi wanatuamini,pamoja na taarifa za uongo ambazo hazina uhakika .
"Ninaposikia askari analalamikiwa huwa inaniumiza sana na lazima nimuite nizungumze nae na ninakuwa mkali sana katika hilo,taafifa za uongo halkadhalika tukikukamata umezusha la kuzusha huko huna uhakika kwakweli tutakushughulikia kwa mujibu wa sheria kwani umetupotezea muda kufanya uchunguzi wa jambo hilo kumbe ni uongo tu nyie ni watu wazima usiposti kitu ambacho huna uhakika nacho"alisema Sirro.
Amewataka wananchi kuacha woga pale wanapomkamata muhalifu na kumpeleka kituo cha polisi,watoe ushirikiano kwa jeshi hilo pale ambapo wanatakiwa kwenda kutoa ushahidi mahakamani,ushahidi unapokosekana mtuhumiwa huyo ataachiwa huru.
"Tatizo la watanzania wengi hawana utamaduni wa kwenda kutoa ushahidi mahakamani pale wanapohitajika,tazizo woga mwingi sana jamani Kesi ni Ushahidi na wengine wanaona wanapoteza muda,lazima atolewe ushahidi ili aweze kushtakiwa kwa mujibu wa sheria msibakie kulalamikia jeshi la polisi wamepokea rushwa".alisema
Aidha Sirro amesema kuwa hali kwa Jiji la Dar es salaam ni shwari kwa sasa ameutaja uhalifu ulioongezeka ni ubakaji na ulawiti ambapo matukio mengine kama ya poanya rod ,unyanganyi yamepungua sana,amezungumzia tukio la mauaji ya askari yaliyotokea jana ya Ofisa upelelezi wa wilaya ya Kibiti mkoa wa Pwani Peter Kubezya huko mkoa wa Pwani kibichi amesema wamejipanga kwenda kuwasaidia maana wanayo kazi kubwa ya kuhakikisha usalama wa nchi raia na mali zao ndiyo kazi ya jeshi la polisi "ukiona mwenzio amenyolewa wewe tia maji"



