Na Raymond William. Sungura!, napolisikia jina sungura mawazo yangu yote pamoja na fikra zangu zinanipelekea kukumbuka u...
Na Raymond William.
Sungura!, napolisikia jina sungura mawazo yangu yote
pamoja na fikra zangu zinanipelekea kukumbuka ucheshi na ujanja wa mnyama huyu
katika hadithi mbali mbali enzi zile nikiwa darasa la 4 katika moja ya shule za
mkoa Wa Arusha. Jamanii ! nalikumbuka sanaa shahiri lile la SIZITAKI MBICHI HIZI. Japo kuwa nakumbuka moja ya
Ubeti katika shahiri lile ambalo sungura alisikika akisema.
“SIZITAKI
MBICHI HIZI, Sungura akagumia naona nafanya kazi bila faida kujuayakamtoka
machozi matunda akalilia sungura nakuambia.”
Sungura ni mnyama mwenye sifa kemkem za kuwa mjanja kuliko wanyama wote.
Akuna mtoto wa kizazi hiki ambaye apendi
kufuga sungura ama ajui Hadith ya sungura na wanyama wengine.
Msomaji wangu hapa nitakwenda
kukuelezea jinsi yakufuga sungura {ufugaji wa ndani} ila kuna ufugaji wanje pia
lakini kwa leo tutangazia ufugaji wa ndani. Twende sote….
Lakini Kabla hujaamua kufuga sungura
hakikisha ya kwamba umejitoa na una muda wa kuwahudumia wanyama waha, ufugaji
wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura wanahitaji uangalizi na
hassa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na
mazingira mabaya na machafu
Kuna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale ya kuwafungia ndani muda wote bila kutoka nje na ya pili ni ile ya pili ni nusu nusu yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza kutoka nje kwenye ua maalum, katika aina zote mbili ni muhimu kuhakikisha hakuna upenyo wa kuruhusu panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa sungura.
UFUGAJI WA NDANI
1 - Usitumie banda la kioo kwa sababu halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha
2 - Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha hakuna sehemu zenye ncha kali inayoweza kuwaumiza sungura, kwani wakumia ni mpaka wapone wenyewe au umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic sungura hana uwezo wa kuzimeng'enya na kuisha mwilini mwake, siku ukimchinja atabakia na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa
3 - Ukubwa wa banda usipungue mita 4 * 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa kubwa zaidi ni vizuri
4 - Chini kuwekewe matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini maranda yatokanbayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi hayafai, wawekee kipande cha blanket au taulo la zamani kwa ajili ya kulalia na kujifungulia hasa kwa wazazi
5 - Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara wanapohisi hatari, unaweza kutumia mbao,Box gumu au plastiki
MAITAJI MUHIMU YAKUJUA KIPINDI CHA UFUGAJI.
Tumia mabakuli ya kigae, usiweke vya plastiki maana huvitafuna na kuwaathiri au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku na vyombo visafishwe kila siku
Wapewe majani makavu kwani muhimu sana kwa ajili ya mfumo wa kumeng'enya chakula, mabaki ya mboga za jikoni baada ya kuchambuliwa, pia unaweza kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers mash) kwenye vyombo maalum kama chakula chenye virutubisho Kiasi cha protini wanachohitaji ni 17%
Kila siku jaribu kuondoa uchafu kama vyakula vilivyo mwagika, na kinyesi kilichoganda kwenya matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau mara moja kwa wiki, manyoya ya sungura mzazi yasiondolewe hii huonyesha kwamba anakaribia kujifungua watoto
Wakati mwingine meno ya mbele hukua sana na kumsababishia usumbufu wakati wa kula, waone wataalam ukiona ni marefu zaidi na yanahitaji kupunguzwa, dalili kuu ni sungura kushindwa kula kwa zaidi ya masaa 12
Miguu ya sungura si kama ya wanyama wengine, nyayo zake zimefunikwa kwa manyoya, angalia ukiona yananyonyoka kuna tatizo chunguza, kucha zake zinahitaji kupunguzwa zikikua sana waone maofisa ugani wa mifugo wakusaidie kwa hili
Usimbebe kwa kutumia masiki yake huwa wanaumia sana, shika ngozi nyuma ya shingo kama paka ukitaka kumbeba na pia weka mkono mmoja kwa chini ili kusapoti uzito
Wapewe dawa ya minyoo kama piperazine kila baada ya miezi mitatu, dawa za wadudu kama akheri powdeer zinyunyuziwe kwenya mabanda yao kuzuia viroboto, usiwape dawa nyingine bila ushauri wa kitaalamu, antibiotics ndio usijaribu kabisa kama nilivyosema mwanzo
Kwa kufika hapa natumaini umepata kujua namna ya kumfuga
mnyama huyu ambaye ni mjanja sana kwa tabia yake ambayo hata watoto wadogo
huwapenda kwaajili ya ujanja wake tukutane tena kesho katika safu hii ya Dira
kuu. KWA MAONI NA USHAURI TUPIGIE 0754954872.
www.wepesimedia.blogspot.com



