http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Makubwa haya!! Mtu mmoja atiwa mbaroni kwa kujaribu kujikata uume

Jeshi la Polisi mkoani Singida, inamshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 60 kwa tuhuma za kujaribu kujiua baada ya kukata kwa pang...

Jeshi la Polisi mkoani Singida, inamshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 60 kwa tuhuma za kujaribu kujiua baada ya kukata kwa panga uume wake hadi kuutenganisha kabisa na mwili, kwa madai ya kuchoka kuhangaika na ugumu wa maisha unaomkabili.

Mwanaume huyo Ntandu Mahumbi mkulima na mkazi wa Kijiji cha Maghojoa wilaya ya Singida, anadaiwa kutenda kosa hilo juzi saa tano asubuhi, muda mfupi baada ya kurejea nyumbani akitoka kulima shambani.

Alisema mzee Mahumbi amelazwa katika hospitali ya mkoa mjini hapa chini ya ulinzi wa askari polisi,na pindi uchunguzi utakapokamilika, atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ya kutaka kujiawa.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, ACP Debora Magilingimba alisema tukio hilo la kusikitisha, limetokea Februari 23 mwaka huu huko katika kijiji cha Maghojoa
.
Katika tukio la pili, Magiligimba alisema mkulima wa kijiji cha Mwanyonye kata ya Ikhanoda wilaya ya Singida, Salome Mwanga (55) amefariki dunia baada ya kupigwa kichwani kwa jiwe na mtoto wake Ally Ramadhani (30).

Alisema kuwa kifo hicho kimechangiwa na mgogoro wa kugombea shamba.
Kamanda huyo alisema tukio hilo limetokea Februari, 21 mwaka huu saa nne asubuhi huko katika kijiji cha Mwanyonyi kata ya Ikhanoda.

Alisema siku ya tukio, mtuhumiwa Ally alikuwa analima katika shamba lililopo jirani na nyumbani kwao ambalo mama yake pia hulilima.

“Salome alimwendea Ally na kumtaka asiendelee kulima katika shamba hilo,na Ally aligoma na kumwangiza mama yake aondoke haraka hapo shambani.Salome hakuondoka kitendo kilichosababisha Ally aokote jiwe na kumpiga kichwani na kumsababishia kupata jereha na maumivu makali,” alisema Magiligimba.

Alisema Salome aliweza kukimbizwa katika kituo cha afya cha Ilongero kwa ajili ya kupatiwa matibabu.Hata hivyo ilipofika saa mbili usiku,alifariki dunia.
Alisema wanamshikilia Ally na pindi uchunguzi utakapokamilika,atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ya mauaji.

Na Nathaniel Limu, Singida

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Makubwa haya!! Mtu mmoja atiwa mbaroni kwa kujaribu kujikata uume
Makubwa haya!! Mtu mmoja atiwa mbaroni kwa kujaribu kujikata uume
http://dewjiblog.co.tz/wp-content/uploads/2017/02/pingu-gereza-prisons-handcuff-750x375.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/02/makubwa-haya-mtu-mmoja-atiwa-mbaroni.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/02/makubwa-haya-mtu-mmoja-atiwa-mbaroni.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy