http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Mafuriko ya Mvua yabomoa nyumba na Kuua Watu Wanne Mpwapwa- Dodoma

Watu wanne wakiwamo watatu wa familia moja, wamefariki dunia baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko kutokana na mvua iliyonyesha usiku ...


Watu wanne wakiwamo watatu wa familia moja, wamefariki dunia baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko kutokana na mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia jana katika Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.


Hata hivyo, viongozi mbalimbali wametoa takwimu zinazotofautiana kuhusu idadi ya vifo vilivyotokea.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema watu wanane walikuwa wameripotiwa kufariki dunia na kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ilikuwa inajiandaa kwenda eneo la tukio ili kujionea uharibifu uliotokea.


Lakini, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema taarifa alizonazo ni za watu watatu waliopoteza maisha na kwamba bado hajapata taarifa sahihi za tukio ambalo lilitokea katika vijiji vya Mang’angu na Chinyika katika Kata ya Ving’awe.


Akizungumza na waandishi wa habari jana, mmoja wa manusura, Beka Mlami (10) alisema walikuwa wamelala wakiwa watano katika nyumba yao mvua kubwa ilipoanza kunyesha kuanzia saa tatu usiku na ilipofika usiku wa manane nyumba yao iliyojengwa kwa udongo ilisombwa na maji.


Mbali na yeye, wengine waliokuwa katika nyumba hiyo ni Martha Sumisumi (60), Shukuru Donald (15) aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Mwanakianga, Bernadetha Sumisumi (9) aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Ilolo na Joseph Sumisumi (12) ambaye alinusurika.


Beka alisema baada ya kuona maji yameingia ndani, aliwaambia ndugu zake wakimbie watoke nje na wakati wanajiandaa kuvaa nguo nyumba yao ilianguka na kuwaponda, lakini yeye alifanikiwa kutoka na kupanda juu ya bati.


Alisema baada ya kutoka nje ndipo gogo kubwa la mti lililosombwa na maji lilipopiga nyumba yao na kuanguka chini hivyo ndugu zake wengine kushindwa kutoka na hivyo kusombwa na maji.


Alisema baada ya kutoka nje alimwona ndugu yake mwingine Joseph akiwa anapelekwa na maji, lakini alifanikiwa kujiokoa.


Mkazi mwingine wa eneo hilo, Steven Noel alisema nyumba iliyosombwa na maji ilikuwa imejengwa karibu na korongo la maji, hivyo baada ya mvua kunyesha, maji yaliacha mkondo wake na kuingia kwenye makazi ya watu na kusababisha maafa hayo.


“Mvua ilisababisha mafuriko makubwa ambayo yalikuwa yamebeba na magogo makubwa ambayo yaliipiga ile nyumba na kuivunja katikati,” alisema Noel.


Alisema baada ya gogo la mti kuipiga nyumba hiyo, maji yalijaa ndani na kwa kuwa milango ilikuwa imefungwa, yalikosa njia ya kutokea na kuiangusha.


Noel alisema kulipopambazuka, walifukua na kuipata miili ya watu hao watatu huku mwili mwingine wa Jesca Lubeleje (19) mkazi wa Kijiji cha Chinyika ukiokotwa.



COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mafuriko ya Mvua yabomoa nyumba na Kuua Watu Wanne Mpwapwa- Dodoma
Mafuriko ya Mvua yabomoa nyumba na Kuua Watu Wanne Mpwapwa- Dodoma
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiK4X8Cc9_tIqGW2gW9X43eCzQzKiBKuu-NpO0NaxX6C36WW-7ikUJudkm3HGpinEjmIuGDSVQNFcLD6uAAcFdNoYp8HYyTcDyLUW6e9i5YexpeSObZFSamhnBFfYEl1FwAyD77PCZocuM/s640/4.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiK4X8Cc9_tIqGW2gW9X43eCzQzKiBKuu-NpO0NaxX6C36WW-7ikUJudkm3HGpinEjmIuGDSVQNFcLD6uAAcFdNoYp8HYyTcDyLUW6e9i5YexpeSObZFSamhnBFfYEl1FwAyD77PCZocuM/s72-c/4.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/02/mafuriko-ya-mvua-yabomoa-nyumba-na-kuua.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/02/mafuriko-ya-mvua-yabomoa-nyumba-na-kuua.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy