http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

JAFO AWATAKA WANAFUNZI NA WALIMU SHULE YA CHANG'OMBE MANISPAA YA DODOMA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA SHULE

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi Seleman Jafo akifungua mlango ili kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa ambao umekamilika...






Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi Seleman Jafo akifungua mlango ili kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa ambao umekamilika kwa asilimia mia moja.




Mojawapo ya madarasa yaliyokamilika katika shule ya msingi Chang’ombe A Manispaa ya Dodoma. Jumla ya vyumba vya madarasa sita vimejengwa ili kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa katika shule hiyo inayotokana na wingi wa wanafunzi, shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi 2000.




Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo akitoa agizo kwa halmashauri, kamati za shule na mikoa nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kutumia juhudi na maarifa ili kuwaletea wananchi maendeleo kwa haraka. Ameridhishwa na ubora na kasi waliyoitumia kujenga majengo hayo.




Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Seleman Jafo akizungumza na walimu, wanafunzi na Kamati ya shule ya msingi Chang’ombe A Manispaa ya Dodoma alipofanya ziara kujionea maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ambao umekamilka kwa asilimia mia moja. Kulia kwake ni Kaimu Afisa Elimu Mkoa Dodoma Tumsifu Mwasamale na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Nelly kinyaga kushoto kwake ni Diwani Kata ya Chang’ombe Bakari Samweli Fundikira.


...............................................................................................................................

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo amewataka wanafunzi na walimu wa shule ya msingi ya Chang’ombe kutunza na kuitumia miundombinu iliyojengwa ili kuongeza ufaulu katika shule hiyo.

Jafo ametoa kauli hiyo leo alipotembelea shule hiyo ili kukagua utekelezaji wa agizo alilolitoa juu ya kukamilisha ukarabati wa miundombinu katika shule hiyo ifikapo 10 januari, mwaka huu.


Novemba 3, mwaka jana Jafo alitoa agizo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa matundu 20 ya vyoo na vyumba vya madarasa 8 pamoja na ukarabati wa vyumba vya madarasa 2 katika shule ya Chan’gombe A ifikapo januari, 10 mwaka huu kabla ya msimu wa masomo kuanza.

Katika ziara hiyo, Jafo amesema ameridhishwa kwa hatua nzuri ya ukarabati huo na kupongeza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa , kamati ya shule ya Chang’ombe ,walimu na Diwani wa Kata ya Chang’ombe kwa utekelezaji huo.

Amesema shule hiyo inapaswa kuongeza ufaulu wake ili iwe mfano mzuri wa kuigwa kwa shule nyingine .

Amebainisha awali alitoa agizo hilo baada ya kubaini changamoto mbalimbali katika shule ya msingi ya Chang’ombe A .

‘’Maagizo niliyoyatoa yalikuwa magumu sana lakini nia yangu ilikuwa kuwatengenezea mazingira rafiki wanafunzi na walimu , nimefarijika na utekelezaji wake, hali haikua nzuri hapo mwanzo lakini nimefarijika kwa kazi nzuri, muonekano wa madarasa unaridhisha nawapongeza sana’’ amesema Naibu Waziri huyo

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Nelly Kinyaga ameishukuru serikali kwa kuboresha miundombinu ya shule hiyo ambapo awali mazingira ya shule hiyo yalikuwa sio rafiki kwa wanafunzi na walimu kutokana na upungufu wa matundu 20 ya vyoo na vyumba vya madarasa 8.

‘’Kwakweli kulikuwa na changamoto sana wanafunzi walikua wengi na madarasa machache lakini kwasasa hatuna watoto wanaokaa chini na msongamano wa wanafunzi darasani umepungua kwa kiasi kikubwa ,naishukuru serikali na Jafo kwa kutilia mkazo ukarabati wa miundombinu ya shule yetu’’ amesema

Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, Ally Mohamed Swalehe ameishukuru serikali kwa kuboresha miundombinu ya shule hiyo rafiki kwa kuwa itaongeza ufaulu katika mitihani na kuepusha magonjwa ya milipuko shuleni hapo.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : JAFO AWATAKA WANAFUNZI NA WALIMU SHULE YA CHANG'OMBE MANISPAA YA DODOMA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA SHULE
JAFO AWATAKA WANAFUNZI NA WALIMU SHULE YA CHANG'OMBE MANISPAA YA DODOMA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA SHULE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEizTKrwks6aj3aVggqUylPnj-tycsPS7q-gUz4JNQnRMgf-e68quTWNvvpfgq8wZBDSobxMSeW5InlRpE-oRuNpd6ieJf77Fh3U1Tg0CuaT7SQdAfgUbQfkMvHJeZDyOFZdVKr9uAxbBgKs/s640/DSC_1216.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEizTKrwks6aj3aVggqUylPnj-tycsPS7q-gUz4JNQnRMgf-e68quTWNvvpfgq8wZBDSobxMSeW5InlRpE-oRuNpd6ieJf77Fh3U1Tg0CuaT7SQdAfgUbQfkMvHJeZDyOFZdVKr9uAxbBgKs/s72-c/DSC_1216.JPG
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/02/jafo-awataka-wanafunzi-na-walimu-shule.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/02/jafo-awataka-wanafunzi-na-walimu-shule.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy