http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Mpalestina aliyeua wanajeshi Jerusalem aliunga mkono Islamic State

Bw Netanyahu amesema njia zilizotumiwa na mshambuliaji ni sawa na zilizotumiwa Nice na Berlin Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amese...

Bw Netanyahu amesema njia zilizotumiwa na mshambuliaji ni sawa na zilizotumiwa Nice na Berlin

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuna dalili kwamba mwanamume aliyevurumisha lori kwenye umati wa watu na kuua wanajeshi wanne Jerusalem alikuwa mfuasi wa kundi linalojiita Islamic State (IS).

Hata hivyo, hajatoa ushahidi wowote kufafanua hilo.

Mwanamume Mpalestina alipigwa risasi na kuuawa.

Mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri kuhusu usalama umeidhinisha kuzuiliwa bila kufunguliwa mashtaka kwa watu wanaoshukiwa kuwa waungaji mkono wa IS.

Mawaziri hao pia wameagiza nyumba ya mshambuliaji huyo ibomolewe haraka iwezekanavyo.

Kundi la Hamas, ambalo linadhibiti ukanda wa Gaza, limesifu shambulio hilo na kulitaja kama hatua ya kupinga hatua ya Israel kuendelea kudhibiti maeneo ya Ukingo wa Magharibi.
Mshukiwa wa shambulizi la Berlin auawa Italia
Mshambuliaji avurumisha lori kwa wanajeshi Israel

Wanawake watatu na mwanamume, wote ambao ni vijana wa miaka 20 hivi, waliuawa kwenye shambulio hilo.

Watu wengine 17 walijeruhiwa, polisi wamesema.

Mshambuliaji ametambuliwa kuwa Fadi Qunbar, 28, kutoka mtaa wa Kipalestina wa Jabel Mukaber mashariki mwa Jerusalem karibu na eneo la shambulio.Jamaa wa Fadi Qunbar akionyesha picha yake kwa wanahabari

Kanda za kamera za CCTV zinaonesha lori likiendeshwa kwa kasi kuelekea walikokuwa wanajeshi hao na kisha kuendeshwa kurudi nyuma kuwaponda.

"Aliendesha lori hilo kurudi nyumba ili kuponda watu zaidi," Leah Schreiber, ambaye alishuhudia shambulio hilo, aliwaambia wanahabari.

"Hilo lilikuwa wazi kabisa."

Jeshi la Israel limesema waliouawa ni Yael Yekutiel, 20; Shir Hajaj, 22; Erez Orbach, 20 na Shira Tzur, 20.

Wanajeshi wengine walimpiga risasi na kumuua Qunbar.

Watu tisa walikamatwa kuhusiana na shambulio hilo, wakiwemo jamaa watano wa mshambuliaji.

Bw Netanyahu alitembelea eneo la shambulio Jumapili alasiri na kusema: "Tunafahamu kwamba kumekuwa na msururu wa mashambulio ya kigaidi.Wanajeshi wakumbatiana eneo la shambulio

"Bila shaka, huenda uka uhusiano fulani - kuanzia Ufaransa hadi Berlin, na sasa Jerusalem."

Washambuliaji Nice na Berlin walitumia njia sawa, ya kuvurumisha lori kwenye umati wa watu.
Watu 12 wafa katika shambulio la lori

Mkuu wa polisi wa taifa Roni Alseich amesema kuna uwezekano dereva huyo alichochewa na shambulio la mwezi uliopita mjini Berlin.

Kabla ya kisa cha Jumapili, wanajeshi 35 walikuwa wameuawa kwa njia mbalimbali na Wapalestina au Waarabu raia wa Israel tangu Oktoba 2015.

Zaidi ya Wapalestina 200 wameuawa katika kipindi hicho.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mpalestina aliyeua wanajeshi Jerusalem aliunga mkono Islamic State
Mpalestina aliyeua wanajeshi Jerusalem aliunga mkono Islamic State
http://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/D91D/production/_93318555_netanyahu.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/01/mpalestina-aliyeua-wanajeshi-jerusalem.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/01/mpalestina-aliyeua-wanajeshi-jerusalem.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy