http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Waziri Mkuu Akabidhi Pikipiki 200 Kwa Vijana wa Arusha ..........Asema Watumishi wa Umma Watakaobainika Kula Fedha Za Miradi Watatimuliwa

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli inasimamia nidhamu ya kazi na heshima kwa wananchi, hiv...



WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli inasimamia nidhamu ya kazi na heshima kwa wananchi, hivyo kutaka kila mmoja atimize wajibu wake.


Aidha, imeonya kuwa fedha za miradi ya serikali ni za moto hivyo ziachwe sifanye shughuli zilizokusudiwa, kwani zikichezewa lazima zitaunguza mtu au watu.


Aliyasema hayo jana jioni alipozungumza na wananchi wa Jiji la Arusha waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.


Alisema serikali imeamua kupanua wigo wa kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika na serikali yake kwa kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali.


Alisema serikali inaendelea kuwahudumia wananchi na kuwataka wakurugenzi, wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia maendeleo ya wananchi huku akimpongeza Gambo kwa kufanya kazi za kuwahudumia wananchi.


Pia amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kukutana na watoa huduma wa magari ya Noah yanayosafirisha abiria maeneo mbalimbali ili kutatua changamoto zao ikiwemo usumbufu wa usafirishaji wanaopata.


Alimpongeza kwa kuwezesha kuibua ajira kwa vijana na kumwagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia kuhakikisha vijana wanapewa maeneo ya kufanya biashara.


Waziri Mkuu pia alitoa rai kwa Halmashauri ya Jiji la Arusha kuangalia jinsi ya kukusanya ushuru kwa kinamama wafanyabiashara wanaotembeza bidhaa zao kwenye mabeseni jijimo humo ili waweze kujikwamua.


Katika mkutano huo, Waziri Mkuu alikabidhi pikipiki zaidi ya 200 kwa waendesha bodaboda ili waweze kujikwamua kiuchumi. Awali, kabla ya Waziri Mkuu kuzungumza na wananchi, Gambo alimpongeza Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro (Chadema) kwa kuungana na falsafa ya Hapa Kazi Tu.


Alisema alipoingia mkoani hapo alikuta Diwani analipwa Sh 150,000 kila mwezi na vocha ya simu Sh 100,000.


“Tuliona hili hapana na tulikata fedha hizo za madiwani tukalipa madeni ya walimu. Kuhusu maeneo ya wazi, tumempa orodha Rais ya hayo maeneo na tunasubiri maamuzi yake kwa ajili ya miradi ya maendeleo,” alisema.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Waziri Mkuu Akabidhi Pikipiki 200 Kwa Vijana wa Arusha ..........Asema Watumishi wa Umma Watakaobainika Kula Fedha Za Miradi Watatimuliwa
Waziri Mkuu Akabidhi Pikipiki 200 Kwa Vijana wa Arusha ..........Asema Watumishi wa Umma Watakaobainika Kula Fedha Za Miradi Watatimuliwa
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEin94iKHsqVfFr57g5WfTOLgwof1c6E-ZsMt8rgTsYXcoMZuWJKT_28pfCeB4O2oIBT802lVWQ23Mut3-l9S0Oy34BPm4olkwtem2gqAodDY0HQFEyuMkwzP0Eicdp7HHe9WuZnxsC6jA4/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEin94iKHsqVfFr57g5WfTOLgwof1c6E-ZsMt8rgTsYXcoMZuWJKT_28pfCeB4O2oIBT802lVWQ23Mut3-l9S0Oy34BPm4olkwtem2gqAodDY0HQFEyuMkwzP0Eicdp7HHe9WuZnxsC6jA4/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/12/waziri-mkuu-akabidhi-pikipiki-200-kwa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/12/waziri-mkuu-akabidhi-pikipiki-200-kwa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy