http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Watoto Watatu Wafa Wakiogelea Bwawani

Watoto watatu wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 12 wamekufa maji baada ya kuzama katika bwawa lililopo eneo la Ziwamboga, Mombasa wila...



Watoto watatu wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 12 wamekufa maji baada ya kuzama katika bwawa lililopo eneo la Ziwamboga, Mombasa wilaya ya Magharibi B, mjini Unguja.


Taarifa ya vifo hivyo imetolewa na daktari wa uchunguzi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Msafiri Marijani.


Daktari huyo alisema watoto hao walikufa baada ya kukosa hewa ya oksijeni baada ya kuzama katika bwawa hilo.


Miili ya watoto hao wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 12 ilifikishwa katika hospitali kuu wa Mnazi Mmoja mjini Unguja majira ya saa sita na nusu mchana.


Kwa mujibu wa taarifa ya polisi kutoka mkoa wa Mjini Magharibi, watoto waliokufa ni Ahmed Mjaka Kombo, Fessal Abrazak Mjaka na Mundhir Sheha Khamis wote wakazi wa Ziwamboga, Mombasa Mjini Unguja.


Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema watoto hao walifika katika bwawa hilo kwa lengo la kuogelea ambapo wawili walizidiwa maji na kuanza kuzama ambapo yule wa tatu aliwafuata wenziwe kwa lengo la kuwaokoa na yeye kuzama.


Imeelezwa kuwa ni kawaida ya watoto kuogolea kwenye bwawa hilo, japo huzuiwa.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B, Silima Haji amewataka wananchi kuacha shughuli za uchimbaji mchanga katika maeneo yasiyo rasmi ili kuepusha matukio yanayozuilika huku diwani wa wadi ya Mombasa akitoa mwito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwazuia watoto wao kucheza katika madimbwi ya maji.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Watoto Watatu Wafa Wakiogelea Bwawani
Watoto Watatu Wafa Wakiogelea Bwawani
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjqof-AUzcwGL1d3ruR9XSofkHZ_KMrjn_sgt2HuDCFh8maGoKzr20e_-DcPB2Ychsr2rMDbeahBqlYF79YDPLL2EJsdNua1AOgmmic7EVhfDQsCoXBhJPjTlsQRRs6vBGYV5KM8O9OsjA/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjqof-AUzcwGL1d3ruR9XSofkHZ_KMrjn_sgt2HuDCFh8maGoKzr20e_-DcPB2Ychsr2rMDbeahBqlYF79YDPLL2EJsdNua1AOgmmic7EVhfDQsCoXBhJPjTlsQRRs6vBGYV5KM8O9OsjA/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/12/watoto-watatu-wafa-wakiogelea-bwawani.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/12/watoto-watatu-wafa-wakiogelea-bwawani.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy