http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Aliyekuwa mbunge wa Rufiji na daktari bingwa wa moyo, Prof. Mtulia afariki dunia

Profesa Idris Mtulia aliyefariki dunia jana, ameacha pengo katika sekta ya afya huku wagonjwa zaidi ya 20 wakimsubiri awafanyie upasuaji...



Profesa Idris Mtulia aliyefariki dunia jana, ameacha pengo katika sekta ya afya huku wagonjwa zaidi ya 20 wakimsubiri awafanyie upasuaji.


Daktari wa Hospitali ya Tumaini, Profesa Chalonde Yongolo (aliyewahi kufanya kazi na Profesa Mtulia) alisema licha ya kuwa mwalimu wake, alikuwa akishirikiana naye kufanya kazi hospitalini hapo.


Profesa Mtulia (pichani) aliyefariki dunia ghafla nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam jana asubuhi imeelezwa alikuwa mchapakazi, mwenye maadili msaada mkubwa kwa jamii.


“Ni pigo kubwa, leo alikuwa na wagonjwa 20 ambao walitarajia kupata huduma ya upasuaji. Nimepokea taarifa za msiba huu saa sita mchana na kwa mujibu wa mke wa marehemu kifo chake ni cha ghafla kwa kuwa aliamka salama na alipata kifungua kinywa na akaenda kupumzika na kupitiwa na mauti.”


Profesa Mtulia aliwahi kuwa mbunge wa Rufiji na Mwenyekiti wa Bodi ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD).


Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema licha ya kuwa alikuwa amemaliza muda wake lakini Profesa Mtulia aliitumikia bodi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.


“Bado alikuwa mshauri katika mambo mbalimbali yahusuyo bodi.”

Bwanakunu alisema Profesa Mtulia alikuwa mchangamfu, mcheshi na huru kuzungumza na watu wote pasipo kujali rika.


“Hakuwa mtu wa kawaida, alikuwa daktari hivyo alifanya majukumu yake kama mtu anayeelewa vizuri kitu anachokifanya na hata baada ya kumaliza muda wake mchango wake ulikuwa ni muhimu.


"Alikuwa mtaalamu wa afya, msikivu na mpenda haki aliyehakikisha watu wanapata huduma kwa muda mwafaka."

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Aliyekuwa mbunge wa Rufiji na daktari bingwa wa moyo, Prof. Mtulia afariki dunia
Aliyekuwa mbunge wa Rufiji na daktari bingwa wa moyo, Prof. Mtulia afariki dunia
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh4cd0B7dLWaT08EAXcauMX2IjhZEnsXzdlimZ7avbP-EBvwgdliKO4yunhI-wTPbCOth-7qC83zErAw2QWq4PA9o8HsyH73mC6JdtPzOI82JOV_vSU6nxI1WALbOLk9MrsMqsps-nLzuY/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh4cd0B7dLWaT08EAXcauMX2IjhZEnsXzdlimZ7avbP-EBvwgdliKO4yunhI-wTPbCOth-7qC83zErAw2QWq4PA9o8HsyH73mC6JdtPzOI82JOV_vSU6nxI1WALbOLk9MrsMqsps-nLzuY/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/12/aliyekuwa-mbunge-wa-rufiji-na-daktari.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/12/aliyekuwa-mbunge-wa-rufiji-na-daktari.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy