http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA GEREZA LA UKONGA DAR ES SALAAM LEO SOMA ALICHOKINENA.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kust...


Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016

Mkuu wa gereza la Ukonga akieleza changamoto za kazi Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo
Novemba 29, 2016.

Askari wakiwa na shauku ya kutoa kero zao mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli alipoongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016



Baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Rais Dkt John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akichukua maelezo kutoka kwa maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016.

Mmoja wa askari wa Kikosi Maalumu cha Magereza wakitoa kero zao mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016.


Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikaribishwa na Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja ili aongee na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016.


Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipewa muhtasarai wa kazi na Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016


Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kitabu cha wageni akiwa na Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
PICHA NA IKULU.
…………………………………………………………………

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu: 255-22-2114512, 2116898

E-mail: press@ikulu.go.tz

Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,

IKULU,

1 BARABARA YA BARACK OBAMA,

11400 DAR ES SALAAM.

Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 29 Novemba , 2016 (Jumanne) amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar Es Salaam na kupiga marufuku uuzwaji wa sare za majeshi nchini na watu binafsi na kutaka wale wote wanaouza sare hizo wazikabidhi kwa majeshi husika mara moja.

Rais Magufuli amepiga marufuku hiyo kufuatia maelezo kutoka kwa baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza kuwa wamekuwa wakinunua sare za jeshi hilo kutoka kwa watu binafsi kinyume na taratibu za majeshi nchini na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua mara moja wale wote watakaobainika kuuza sare za majeshi ya hapa nchini

Hali kadhalika Rais magufuli amepiga marufuku kwa majeshi yote nchini kuingia ubia na watu binafsi kupangisha ama kuuza maeneo yao kwa ajili ya kufanya biashara na kutaka maeneo yote ya majeshi yabaki katika jeshi husika.



‘‘Haiwezekani sare za majeshi yetu hapa nchini kuuzwa na watu binafsi hilo haliwezekani kamwe labda baada ya kumaliza muda wangu , amesema Rais magufuli”



Aidha Rais Magufuli ametoa shilingi Bilioni Kumi kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kujenga nyumba mpya zitakazotumika kwa ajili ya makazi ya askari wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Ukonga jijini DSM.



Hatua hiyo inafuatia kilio cha askari Magereza kuwa wengi wao wamekuwa wakiishi uaraiani kitu ambacho ni tofauti na taratibu za majeshi nchini na hata kuzorotesha utendaji kazi wa askari wa Jeshi hilo.





Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. John Pombe Magufuli pia ameagiza Jeshi la Magereza kuhakikisha wafungwa wanatumika katika uzalishaji mali badala ya mfumo wa sasa ambapo baadhi ya wafungwa wamekuwa wakitutumia rasilimali za serikali bila kuzifanyia kazi.



Rais Magufuli amewahakikishia Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kuwa serikali itaendelea kuboresha maslahi yao na vitendea kazi kama inavyofanya kwa majeshi mengine nchini.







Jaffar Haniu

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar Es Salaam

29 Novemba, 2016

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : RAIS DKT MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA GEREZA LA UKONGA DAR ES SALAAM LEO SOMA ALICHOKINENA.
RAIS DKT MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA GEREZA LA UKONGA DAR ES SALAAM LEO SOMA ALICHOKINENA.
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2016/11/GER-300x123.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/11/rais-dkt-magufuli-afanya-ziara-ya.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/11/rais-dkt-magufuli-afanya-ziara-ya.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy