http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

WAZIRI MKUU ACHOSHWA NA MADUDU BODI YA KOROSHO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ahutubia wananchi wa wilaya ya Nachingwea katika kiwanja cha Sokoine waziri mkuu alipokea malalamiko kutoka kwa ...





Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ahutubia wananchi wa wilaya ya Nachingwea katika kiwanja cha Sokoine waziri mkuu alipokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusiana na biashara ya korosho Ikamlazimu waziri mkuu kumuagiaza Waziri wa kilimo afanye mapitio makini kweznye bodi nzima ya korosho



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa apokea hundi ya mfano ya zaidi shilingi milioni kumi nasita kutoka kwa Mkuu wa Mkoa walindi kwa ajili ya Rambirambi kwa wananchi wa mkoa wa Kagera kulia kwa waziri mkuu ni mkewe Mary Majaliwa waziri mkuu yupo mkoani Lindi katika ziara ya kikazi katika wilaya ya Nachingwea na Ruwangwa

Picha na Chris Mfinanga

………………………………………………………………………………………………..

*Aagiza ifanyiwe marekebisho makubwa

*Aishangaa kung’ang’ania minada

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba kuifanyia marekebisho makubwa Bodi ya Korosho na menejimenti yake baada ya kushindwa kusimamia zao hilo ipasavyo.

Amesema Serikali itafanya mapitio ya bodi zote za mazao ya biashara na imeanza na zao la korosho kisha zao la pamba, tumbaku, kahawa, katani na chai. Katika tathmini na mapitio hayo , bodi itakayobainika kushindwa kutekeleza majukumu yake itavunjwa.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Oktoba 16, 2016) wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja cha Sokoine wilayani Nachingwea mkoani Lindi.

Alisema anaishangaa bodi hiyo kuacha kutekeleza majukumu yake na kuingilia minada ya korosho na kuzuia baadhi ya wafanyabiashara wasiweze kununua zao hilo hali inayoashiria kuwepo kwa watu waliopangwa kununua bila ya kufuata utaratibu.

“Bodi leo wamejipa jukumu la kusimamia minada ! sio kazi yao ni kazi ya chama kikuu, zao la korosho linalimwa kutoka mkoani Ruvuma hadi Tanga, mtasimamia minada mingapi viachieni vyama vikuu. Vyama vikuu vikiharibu walalamikaji waje kwenu kama sehemu ya rufaa. Sasa nyinyi mnasimamia minada mnaharibu walalamikaji watakwenda kwa nani ? kwa nini mng’ang’anie kwenda kwenye minada,” alihoji Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu alisema Ijumaa (Oktoba 14,2016) bodi hiyo ilisitisha mnada wa korosho Lindi kwa sababu wanunuzi hawakuweka bondi (dhamana ya mauzo) na alishatoa maagizo ya kuwataka wanunuzi wasiruhusiwe kununua hadi waweke asilimia 25 ya malipo.

Alisema maagizo hayo aliyatoa tangu mwezi Aprili ila watendaji wa bodi hiyo hawakuyafanyia kazi kwa wakati na badala yake waliwazuia wafanyabiashara waliotaka kununua korosho Lindi kwa madai ya kutokuwa na bondi huku wakiwaruhusu wa Mtwara.

“Kama kule walinunua bila bondi kwa nini wasiwaruhusu na Lindi wakanunua bila bondi ili nijue kwamba mliamua kugoma kuteleza maelekezo ya Serikali? Au hamkumtaka aliyeshinda nyie mlikuwa mnamtaka nani nitashughulika na nyie,” alisisitiza.

Aliongeza kuwa “Nimesema tukitoa maelekezo lazima yatekelezwe na atakayeshindwa hatufai, Mheshimiwa mbunge umelalamika juu ya bodi hawa ndio wabeba maelekezo hatujawahi kuona bodi ya korosho ikienda vijijini kuzungumza na vyama vikuu hata mara moja,”.

Akizungumzia kuhusu suala la wakulima kulazimishwa kufungua akaunti za kupitishia malipo yao alisema wasiwalazimishe.“Waelimisheni wakulima umuhimu wa kufungua akaunti lakini si kwa kuwalazimisha wote wawe na akaunti hadi yule mwenye kilo tano…na akaunti yenyewe inafunguliwa kwa sh. 100,000,” alisema.

Alisema “’wanashindwa kutekeleza niliyowaagiza, halafu wanasingizia utendaji wao mbovu kuwa ndio maagizo yangu,’ niliwaagiza wapi,” alihoji na kuongeza kuwa “yapo makundi yanafanya mambo yanavyotaka alafu yakiwazidi mambo wanasingizia viongozi wajuu na ndio wale wanaosema kila kitu nimeagizwa kutoka juu, juu wapi?

“Lazima tuendelee kudhibiti nidhamu ya vyombo vya tunavyoviunda kwa ajili ya kuwahudumia wananchi. Tutaendelea kusimamia nidhamu kwa taasisi zinazowahudumia wakulima nchi nzima,” alisisitiza.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alimkabidhi Waziri Mkuu msaada wa sh. milioni 16.3 pamoja na nguo kwa ajili ya kusaidia wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : WAZIRI MKUU ACHOSHWA NA MADUDU BODI YA KOROSHO
WAZIRI MKUU ACHOSHWA NA MADUDU BODI YA KOROSHO
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2016/10/kimo1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/10/waziri-mkuu-achoshwa-na-madudu-bodi-ya.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/10/waziri-mkuu-achoshwa-na-madudu-bodi-ya.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy