http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Simu ya Samsung yashika moto kwenye ndege

Simu ya kampuni ya Samsung aina ya Galaxy Note 7, ambayo ilikuwa imethibitishwa na kampuni hiyo kuwa ilikuwa salama, imeshika moto kwenye n...





Simu ya kampuni ya Samsung aina ya Galaxy Note 7, ambayo ilikuwa imethibitishwa na kampuni hiyo kuwa ilikuwa salama, imeshika moto kwenye ndege nchini Marekani.

Simu hiyo inadaiwa kushika moto ikiwa na abiria aliyekuwa kwenye shirika la ndege la Southwest Airlines.

Shirika hilo limesema abiria waliokuwa kwenye ndege moja yake, iliyokuwa imepangiwa kusafiri kutoka Louisville, Kentucky, hadi Baltimore, Maryland, waliondolewa kwenye ndege kwa dharura kabla ya ndege hiyo kupaa Jumatano.

Kampuni ya Samsung iliwashauri watu waliokuwa wamenunua simu za Note 7 kuzirejesha kwa kampuni hiyo baada ya kugunduliwa zilikuwa na tatizo kwenye betri zake.

Samsung imesema bado inachunguza kisa hicho cha Jumatano.
Panasonic yatengeza betri inayojipinda
Samsung: Kiwanda chetu hakina madhara
Samsung yasitisha uuzaji wa Galaxy Note 7

"Tunashirikiana na maafisa wa serikali na maafisa wa shirika la Southwest kupata simu hiyo na kuthibitisha chanzo (cha moto huo)," kampuni hiyo imesema kupitia taarifa.

Msemaji mmoja wa shirika la Southwest Airlines amemabia BBC: "Abiria mmoja alitufahamisha kuhusu moto uliokuwa unafuka kutoka kwa simu. Abiria wote na wahudumu wa ndege waliondolewa salama kutoka kwenye ndege."




Mmiliki wa simu hiyo Brian Green, akizungumza na Jordan Golson wa shirika la The Verge, amesema alinunua simu hiyo tarehe 21 Septemba.
Kwa nini betri za Lithium hulipuka?

Amesema simu hiyo ilikuwa na alama ya mraba ya rangi nyeusi kwenye pakiti yake, alama ambayo iliongezwa na Samsung kutofautisha kati ya simu zilizokuwa zimeuzwa awali ambazo zilidaiwa kutokuwa salama na simu mpya zilizokuwa zimechunguzwa.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Simu ya Samsung yashika moto kwenye ndege
Simu ya Samsung yashika moto kwenye ndege
http://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/1B3D/production/_91537960_whatsubject.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/10/simu-ya-samsung-yashika-moto-kwenye.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/10/simu-ya-samsung-yashika-moto-kwenye.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy