http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

WATATU WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI ARUSHA KWA K0SA LA KUGHUSHI NYARAKA ZA SERIKALI.

  Na Mahmoud Ahmad,Arusha Jeshi la polisi mkoani Arusha linawashikilia watu watatu kwa kosa la kughushi nyaraka za ofisi na kupelekea wizi...

 kamanda-charles-mkumbo

Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Jeshi la polisi mkoani Arusha linawashikilia watu watatu kwa kosa la kughushi nyaraka za ofisi na kupelekea wizi wa jumla ya kiasi cha sh,50 milioni mali ya chama cha wakulima cha Tanganyika(TFA).

Kushikiliwa kwa watuhumiwa hao kunakuja zikiwa ni siku chache tu baada ya jeshi hilo kumshikilia na kisha kumwachia kwa dhamana aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya muda wa TFA ,Meynard Swai kwa tuhuma za ubadhirifu wa mali na fedha ndani ya chama hicho.

Mwenyekiti huyo alishikiliwa kwa siku kadhaa na jeshi la polisi mkoani hapa mwezi uliopita jijini na kisha kuhojiwa kabla ya kuachiwa kwa dhamana ambapo kwa sasa polisi bado wanaendelea na uchunguzi dhidi ya mashtaka yanayomkabili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha,Charles Mkumbo alisema kwamba watuhumiwa hao walishikiliwa katika maeneo tofauti hapa nchini.

Aliwataja kwa majina walioshikiliwa kuwa ni Salvatory Mwandu,Simon Mwandu pamoja na mkazi wa jijini Dar es salaam,Jesca Canisius ambao kwa sasa wameachiwa kwa dhamana.

Mkumbo,alisema kwamba watuhumiwa hao wako chini ya uchunguzi na jeshi lake na bado linaendelea na upelelezi wa kina huku akisisitiza ya kwamba hawatasita kumchukulia hatua za kisheria mtu yoyote atakayevunja sheria za nchi.

“Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa tuhuma hizo na linatoa rai kwa wananchi wote wa mkoa wa Arusha kuacha vitendo viovu vya kuvunja sheria za nchi ,jeshi la polisihalitasita kuwachukulia hatua za kisheria wanaokiuka taratatibu za kisheria”alisema Mkumbo

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : WATATU WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI ARUSHA KWA K0SA LA KUGHUSHI NYARAKA ZA SERIKALI.
WATATU WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI ARUSHA KWA K0SA LA KUGHUSHI NYARAKA ZA SERIKALI.
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2016/09/kamanda-Charles-Mkumbo.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/watatu-washikiliwa-na-jeshi-la-polisi.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/watatu-washikiliwa-na-jeshi-la-polisi.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy