http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

UVCCM WATOA POLE KWA MAAFA YALIOSABABISHWA NA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA

Majeneza ya miili ya watu waliopoteza maisha jana kutokana na tetemeko la ardhi lililopokea mjini Bukoba mkoani Kagera waombolezaji watatoa ...





Majeneza ya miili ya watu waliopoteza maisha jana kutokana na tetemeko la ardhi lililopokea mjini Bukoba mkoani Kagera waombolezaji watatoa heshima zao za mwisho na kuaga miili ya marehemu hao leo kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ambapo Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa ataongoza wananchi wa Bukoba kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu hao.

…………………………………………………………………………….

NA MWANDISHI WETU

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umetuma salamu za pole wananchi wa mkoa wa Kagera kutokana na vifo vya zaidi ya watu 11 vilivyosababisha na tetemeko la ardhi lililotokea juzi.

Katika salamu hizo zilizotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVVCM, Shaka Hamdu Shaka kwa niaba ya umoja huo, alisema wamepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa ya vifo hivyo.

Alisema tetemeko hilo ni pigo kwa UVCCM na taifa kwa ujumla kwa kuwa limesababisha vifo vya watu ambao ni nguvu kazi ya taifa pia kusababisha hasara kutokana na uharibifu wa mali mbalimbali na makazi.

“UVCCM tumepokea kwa mshituko mkubwa tukio hilo kubwa na zito ambalo limesababisha maafa na hasara kwa taifa,”alisema.

Alisema umoja huo unawaombea marehemu wa tukio hilo wapate pumziko la milele peponi na kuwaombea majeruhi wapone haraka na kurudi kwenye shughuli zao za kawaida.

“Katika kipindi hiki kigumu Jumuia yetu inaungana na Watanzania wengine kuzipa mkono wa pole familia zote zilizopoteza ndugu zao na pia tukiwafariji wote waliopata hasara ya kuharibikiwa nyumba zao na kupoteza mali,”alisema.

Alisema janga hilo ni limemgusa kila mtanzania mwerevu mwenye upendo na uzalendo hivyo linapaswa kuwaweka pamoja Watanzania wote ili kufarijiana na kukabiliana na magumu yaliyotokea.

Aidha, Shaka alisema wanatoa mkono wa pole kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kutokana na vifo hivyo na kasara iliyopatikana.

Shaka aliwashukuru na kuwakupongeza viongozi wa umoja huo walioko mkoani humo wakiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera Yahya Kateme, kwa ushirikiano walioendelea kuutoa baada ya kutokea kwa tukio huilo.

Huu si wakati wa siasa bali ni kipindi kigumu cha kukabili yale yote yaliotokea na kudhuru au kuharibu taaswira iliokuwepo awali ya ustawi wa maisha ya wenzetu ambao wamepatwa na janga hilo.

Kila kijana mzalendo ni vyema akaenda kuripoti kwa viongozi wa maeneo husika aidha wakuu wa wilaya au mkoa ili kupewa maelekezo na miongozo katika kila hatua ya kusaidiana kwa hali na mali wakati wote hadi hali itakaporejea kama kawaida.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : UVCCM WATOA POLE KWA MAAFA YALIOSABABISHWA NA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA
UVCCM WATOA POLE KWA MAAFA YALIOSABABISHWA NA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2016/09/index-27.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/uvccm-watoa-pole-kwa-maafa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/uvccm-watoa-pole-kwa-maafa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy