http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

MKUTANO WA WADAU WA UTALII KUFANYIKA ARUSHA KESHO

Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa siku moja wa wadau wa sekta ya Utal...





Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa siku moja wa wadau wa sekta ya Utalii mkoani Arusha unaotarajiwa kufanyika kesho.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake,amesema kuwa mkutano kama huo ulifanyika kwa mara ya mwisho mwaka 2012 hivyo wameona ni vyema serikali kushirikiana na wadau wa utalii kukaa pamoja kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuboresha sekta hiyo,ambayo asilimia 80% ya watalii wanaoingia nchini hufika mkoani hapa .

Amesema kuwa mkoa wa Arusha ni kitovu cha cha utalii na unachangia pato la mkoa kwa asilimia20% na kitaifa kwa asilimia 17%ambapo mwaka 2015 idadi ya watalii iliyoingia nchini ilikuwa 1,137,182 na kuingizia Taifa kiasi cha dola za kimarekani 1.9 milioni,katikaq idadi hiyo asilimia 80%watalii walitembelea mkoa kwasababu ya vivutio vingi vilivyopo mkoani Arusha.

Amesema kwamba madhumuni ya mkutano huo ni kujadili hali ya maendeleo ya utalii ya mkoa ,fursa zilizopo,mafanikio ,changamoto na kuweka mikakati yakuboresha huduma mbalimbali za utalii ambapo wadau watapata fursa ya kubadilishana mawazo na kuadhimisha siku ya utalii duiaani amabayo huadhimishwa kila mwaka septemba 27.

“Maadhimisho haya ya utalii mwaka huu yamebeba kauli mbiu UTALII KWA WOTE,Kwa kuzingatia hilo wadau mbalimbali wa sekta hiyo ya utalii zikiwemo TANAPA,NCAA,HAT,TTB,TATO,TTGA,TRA,TACTO Watawasilisjha mada ambazo zitalenga kuboresha utalii,pamoja na kuhakikisha elimu na fursa za Utalii zinaifikia jamiii “ alisisitiza Gambo.

Amesema kuwa wadau watakaoshiriki mkutano huo ni wahifadhi,Wakala wa waongozaji watalii,Wakala wa wausafirishaji watalii,watoa huduma za malazi,Bodi ya Utalii,na Viongozi watendaji wa serikali ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe.

Mkutano huo wa siku moja umefadhiliwa na Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA)kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na Ofisi ya Kanda ya Utalii ndiyo waandaaji wa mkutano huo wa wadau mbalimbali wa Utalii Mkoani Arusha

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : MKUTANO WA WADAU WA UTALII KUFANYIKA ARUSHA KESHO
MKUTANO WA WADAU WA UTALII KUFANYIKA ARUSHA KESHO
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2016/09/images-22.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/mkutano-wa-wadau-wa-utalii-kufanyika.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/mkutano-wa-wadau-wa-utalii-kufanyika.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy