http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Majina ya waliofariki katika ajali iliyohusisha basi la Super Shem na Hiace jijini Mwanza

WATU 13 wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha basi la Super Shem lenye namba za usajili T 874 CWE lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea M...




WATU 13 wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha basi la Super Shem lenye namba za usajili T 874 CWE lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Mwanza na Hiace yenye namba T 368 CWQ iliyokuwa ikitoka Jijini Mwanza kuelekea Wilaya ya Kwimba.


Katika ajali hiyo mfanyabaishara ndogo ndogo maarufu machinga, Peter Tobari, aliokoa maisha ya abiria zaidi ya 30 na kumsaidia dereva wa basi la Super Shem ambaye alikuwa amekandamizwa miguu na basi hilo baada ya kugongana na Hiace.


Ajali hiyo imetokea siku mbili baada ya ile ya basi la Kampuni ya New force iliyotokea mkoani Njombe ikihusisha basi lenye namba T 429 DEU lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Songea mkoani Ruvuma, ambapo watu 12 walifariki dunia na wengine 28 kujeruhiwa vibaya. Katika ajali ya Mwanza, gari dogo aina ya Hiace liligongana uso kwa uso na basi la Super Shem na kusababisha vifo hivyo na wengine 10 kujeruhi.


Ajali hiyo imetokea umbali wa mita 200 kutoka kituo kidogo cha mabasi cha Hungumalwa njia panda ya Shelui na Mwamashimba katika Kijiji cha Mwamaya wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Ilielezwa katika tukio hilo, dereva wa Hiace aliingia barabara kuu ya Mwanza-Shinyanga bila kuchukua hadhari na hivyo kukutana na basi hilo.


Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema baada ya ajali hiyo watu 10 walikufa papo hapo na wengine 11 kujeruhiwa, ambapo mmoja alifariki dunia akiwa njiani akipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Kwimba na wawili walifariki dunia wakati wakipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi kwa matibabu zaidi.


Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kwimba, Dk. Bethod Nchemba, akizungumzia ajali hiyo alisema walipokea majeruhi 10 wakiwemo wanaume na wanawake watano ambapo mmmoja alikuwa na hali mbaya na alifariki akiwa mapokezi wakati akiendelea kupewa huduma.


Aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Monica Shija, Christina Costantine, Theresia Majenga wote wakiwa wakazi wa Kijiji cha Gulumwa wilayani Kwimba, Lwinzi Kope mkazi wa Kijiji cha Chaselwe, Mabula Magi wa Rukwa, Isaya Deogratius mkazi wa Mbande, Moses Kamel wa Kijiji cha Bupamwadomu, George Ndila mkazi wa Sangu, Kondakta wa hiace aliyefahamika kwa jina moja la Poni pamoja na mtu mmoja mwanaume, mama mmoja na mtoto ambao hawajafahamika wote wakiwa ni abira wa Hiace.


Alisema majeruhi watatu wanaendelea vizuri na matibabu katika hospitali hiyo na miili tisa kati ya 11 imeshatambuliwa isipokuwa mwili wa mama mmoja na mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 5 na majeruhi sita wamelazimika kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Majina ya waliofariki katika ajali iliyohusisha basi la Super Shem na Hiace jijini Mwanza
Majina ya waliofariki katika ajali iliyohusisha basi la Super Shem na Hiace jijini Mwanza
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhjkl9lUDGKZxLQpB__5mY1GGbkUb7rXtIATFS57B51h_EKanbOAc194CrZQMlSVhq6k3-RFaAethz6HB2M_YWSepwcL4Yc1K2K6hyphenhyphenwvs_95lEzwlEOXVoc1ki8YSf79csqVRFU2XC1Mg8/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhjkl9lUDGKZxLQpB__5mY1GGbkUb7rXtIATFS57B51h_EKanbOAc194CrZQMlSVhq6k3-RFaAethz6HB2M_YWSepwcL4Yc1K2K6hyphenhyphenwvs_95lEzwlEOXVoc1ki8YSf79csqVRFU2XC1Mg8/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/majina-ya-waliofariki-katika-ajali.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/majina-ya-waliofariki-katika-ajali.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy