http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Korea Kaskazini yafanya 'jaribio kubwa la nyuklia'

Image copyrightAP Korea Kaskazini inadaiwa kutekeleza jaribio la tano na kubwa zaidi la kifaa cha nyuklia, maafisa wa jeshi la Korea Kusini ...

Image copyrightAP

Korea Kaskazini inadaiwa kutekeleza jaribio la tano na kubwa zaidi la kifaa cha nyuklia, maafisa wa jeshi la Korea Kusini wamesema.

Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye ametaja jaribio hilo kuwa "jaribio la kujiangamiza" ambalo linaonyesha "kutomakinika" kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Maafisa wa Seoul wanasema mitambo yao iligundua tetemeko la ardhi ya nguvu ya 5.3 kwenye vipimo vya Richter karibu na eneo ambalo Pyongyang hutumia kufanya majaribio ya vifaa vya nyuklia.

Korea Kaskazini kufikia sasa haijasema lolote kuhusu jaribio hilo, lakini wachanganuzi wanasema hii huenda ikawa ishara ya hatua zilizopigwa na taifa hilo katika kustawisha teknolojia yake ya nyuklia.
Waziri aliyesinzia mkutanoni auawa Korea Kaskazini

Mitetemeko ya ardhi ya kusababishwa na binadamu ambayo imetokea eneo hilo awali yote ilitokana na majaribio ya nyuklia.

Bi Park, ambaye amesitisha ghafla ziara yake ng'ambo, amesema baada ya kutekeleza jaribio hilo la tano la nyuklia "serikali ya Kim Jong-un itakaribisha vikwazo zaidi na kutengwa zaidi na jamii ya kimataifa."

"Uchokozi kama huu utaongeza kazi safari yake ya kuelekea kwenye maangamizi."Image copyrightAFPImage captionMaafisa wa Japan wanasema mitetemeko ya ardhi isiyo ya kawaida ilisikika

Kupitia taarifa iliyotumwa na shirika la habari la Korea Kusini Yonhap, mkuu wa majeshi ya Korea amesema: "Tunakadiria kwamba Kaskazini imetekeleza jaribio kubwa zaidi."

Jaribio hilo linadaiwa kuzalisha nguvu ya kilotani 10, nguvu mara dufu ya jaribio lililotekelezwa Januari.

Wakati huo, Korea Kaskazini ilisema ilikuwa imtekeleza jaribio la bomu la haidrojeni.

Maafisa wa jiolojia wa Marekani, ambao hufuatilia shughuli chini ya ardhi, walisema awali kwamba mitetemeko ilisikika karibu na eneo la Korea Kaskazini la kufanyia majaribio ya nyuklia la Punggye-ri.

Ijumaa huwa ni Siku ya Taifa nchini Korea Kaskazini ambapo taifa hilo huadhimisha kuanzishwa kwa taifa la sasa.

Korea Kaskazini mara kwa mara hutumia majaribio hayo kuonyesha nguvu zake.Image copyrightGEOEYEImage captionEneo la Punggye-ri

Japan imeshutumu jaribio hilo na Waziri Mkuu Shinzo Abe amesema inashirikiana kwa karibu na washirika wake.

Marekani pia imesema inafuatilia taarifa hizo.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Korea Kaskazini yafanya 'jaribio kubwa la nyuklia'
Korea Kaskazini yafanya 'jaribio kubwa la nyuklia'
http://ichef-1.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/1535D/production/_91077868_mediaitem91077695.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/korea-kaskazini-yafanya-jaribio-kubwa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/korea-kaskazini-yafanya-jaribio-kubwa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy