http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Kivutio cha Kimondo kuendela kuongeza mapato ya Serikali

Kimondo kilichopo Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya. …………………………………………………………………………….. Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma. Serikali inaendelea kut...



Kimondo kilichopo Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya.

……………………………………………………………………………..

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma.

Serikali inaendelea kutangaza Kimondo kilichopo Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya ikiwa ni kivutio muhimu na adimu nchini na duniani kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Kamani leo mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Hasungu lililohusu mpango wa Serikali katika kuhamasisha watalii wa ndani na nje kuja kuangalia Kimondo hicho.

Naibu Waziri huyo amesema kuwa Serikali imekuwa inaendelea kuhamasisha kwa kukitangaza Kimondo hicho kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo vipindi vya runinga na nakala za machapisho mbalimbali.

“Uhamasishaji umefanyika kwa kutumia njia mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na vipindi vya runinga vya ZAMADAMU na Utalii wa ndani na kutumia machapisho ya Tanzania ya “The land of great Heritage Sites” na “Tanzania Cultural Heritage Resources” ambapo nakala zake husambazwa katika maonesho mbalimbali na Balozi zetu pamoja na jarida la “Ifahamu Idara ya mambo ya kale”” na jarida la Maliasili,” alifafanua Naibu Waziri huyo.

Aidha, Mhandisi Kamani aliongeza kuwa juhudi hizo limepelekea ongezeko la idadi ya watalii na mapato ambapo kati ya mwaka 2012/2013 na 2014/2015 watalii waliongezeka kutoka 990 hadi 1,681 pamoja na mapato kuongezeka kutoka shilingi 811,000 hadi 2,426,00.

Mbali na hayo, Mhandisi Kamani alitoa wito kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi na wadau wengine kujitokeza kuboresha mazingira na miundombinu ya eneo la kimondo hicho ili kuweza kuzidi kuvutia watalii wengi na kuongeza pato la taifa.

Kimondo hicho kinaendelea kuiweka Tanzania katika ramani ya dunia katika masuala ya utalii ambapo kinaaminiwa kuwa ni kati ya vimondo nane vikubwa zaidi duniani kinachokadiriwa kuwa na uzito wa tani 12, urefu wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo cha mita 1.22.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Kivutio cha Kimondo kuendela kuongeza mapato ya Serikali
Kivutio cha Kimondo kuendela kuongeza mapato ya Serikali
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhNpVQlpCm26vJF_E4-vuZcGyjB52dMFdmdmsZScN_qubgMpcQy_96XGV4yyRE8D6Isf5tPoycHPeMiwLXp-DQswy6Kv_0sT1gS1pwdI6kt7KhjEKF4lF5AAAVM3RsEfMM0immPE-HFzqrx/s640/kimondo-768x576.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhNpVQlpCm26vJF_E4-vuZcGyjB52dMFdmdmsZScN_qubgMpcQy_96XGV4yyRE8D6Isf5tPoycHPeMiwLXp-DQswy6Kv_0sT1gS1pwdI6kt7KhjEKF4lF5AAAVM3RsEfMM0immPE-HFzqrx/s72-c/kimondo-768x576.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/kivutio-cha-kimondo-kuendela-kuongeza.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/09/kivutio-cha-kimondo-kuendela-kuongeza.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy