Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana kwa furaha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa ...
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana kwa furaha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Sala sala nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam.



Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai
nyumbani kwake Sala sala jijini Dar es Salaam alipokwenda kumjulia hali.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Mke wake Mama Janeth Magufuli kushoto akizungumza jambo na Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai nyumbani kwake Sala
sala jijini Dar es Salaam walipokwenda kumjulia hali. Kulia ni mke wa
Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai.


Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia
hali Waziri Mkuu mstaafu John Samuel Malecela ambaye anapata matibabu
jijini Dar es Salaam.

Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akimsalimia Waziri Mkuu mstaafu John
Samuel Malecela ambaye anapata matibabu jijini Dar es Salaam.

Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa pamoja na Rais Dkt. John Pombe
Magufuli akiongoza Sala ya kumuombea Waziri Mkuu mstaafu John Samwel
Malecela pamoja na mkewe Anne Kilango Malecela.

Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na Mke wa Spika Dkt. Fatma
Mganga Ndugai wakati alipokwenda na Rais Dkt. John Pombe Magufuli
kuwajulia hali nyumbani kwao Sala sala jijini Dar es Salaam.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
mke wa Spika Dkt. Fatma Mganga Ndugai huku Mke wa Rais Mama Janeth
Magufuli akiagana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Job Ndugai mara baada ya kuwajulia hali nyumbani kwao Sala sala jijini
Dar es Salaam. PICHA NA IKULU