http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Mwalimu Aliyetuhumiwa Kufanya Mapenzi na Wanafunzi Auawa na Wananchi

Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalic hako MWALIMU Daniel Msalika (42) wa shule ya msingi Nyasosi, wilayani Bariadi, mkoa wa Simiyu am...

Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalic hako

MWALIMU Daniel Msalika (42) wa shule ya msingi Nyasosi, wilayani Bariadi, mkoa wa Simiyu amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando alikokuwa amelazwa akitibiwa majeraha.

Majeraha hayo yalitokana na kushambuliwa na baadhi ya wananchi kwa madai ya kujihusisha kimapenzi na wanafunzi wa kike wa shule hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga aliwaeleza waandishi wa habari jana ofisini kwake kuwa mwalimu huyo alifariki dunia Julai 31 mwaka huu saa nane usiku.

Kamanda Lyanga alisema kuwa siku ya tukio Julai 27 mwaka huu saa 6.30 usiku, wananchi hao ambao idadi yao haijafahamika, walivamia nyumba ya mwalimu huyo baada ya kupata taarifa kuwa kuna mwanafunzi ambaye amelala nyumbani kwake, jambo ambalo halikuwa la kweli.

“Wananchi hao walipata taarifa ya kuwa nyumbani kwa mwalimu kuna mwanafunzi ambaye amelala humo hivyo walimvamia kwa kuvunja mlango na kuanza kumshambulia kwa kutumia silaha mbalimbali za jadi na kumsababishia majeraha makubwa sehemu za kichwani na usoni lakini binti waliyemkuta kwake ni mwenye umri wa miaka 18 na siyo mwanafunzi,” alisema.

Alisema kuwa baada ya uvamizi huo, mwalimu huyo alikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Isanga kupatiwa matibabu, lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, lakini alifariki dunia.

Kamanda alisema kifo chake, kimesababishwa na majeraha ya kushambuliwa huku tuhuma dhidi yake zikiwa si za kweli.

Alitoa mwito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi huku wakisisitiza kuwa wote watakaobainika kusababisha kifo hicho, sheria itachukua mkondo wake.

TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mwalimu Aliyetuhumiwa Kufanya Mapenzi na Wanafunzi Auawa na Wananchi
Mwalimu Aliyetuhumiwa Kufanya Mapenzi na Wanafunzi Auawa na Wananchi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjjMZaDzqFhq3gHddpb2VgT-uoj02N0ljhc_JfdEkwsWkr8XnSTbImRGRgJdhWr6USQsuTzcqu2eWXPbLjosk15HOvufmWl0MxKAsjjOGwUszTiBBRzjHrfd5MbnHMgQfNlfwBTWVRxdc4/s640/ndalichako.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjjMZaDzqFhq3gHddpb2VgT-uoj02N0ljhc_JfdEkwsWkr8XnSTbImRGRgJdhWr6USQsuTzcqu2eWXPbLjosk15HOvufmWl0MxKAsjjOGwUszTiBBRzjHrfd5MbnHMgQfNlfwBTWVRxdc4/s72-c/ndalichako.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/08/mwalimu-aliyetuhumiwa-kufanya-mapenzi.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/08/mwalimu-aliyetuhumiwa-kufanya-mapenzi.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy