Watafiti wanasema hilo ni kaburi la kwanza kabisa la Wafilisti kupatikana W...
Watafiti wanasema hilo ni kaburi la kwanza kabisa la Wafilisti kupatikana
Watafiti wa mambo ya kale nchini Israel wamegundua makaburi ya kwanza ya Wafilisti.Makaburi hayo, yaliyopatikana eneo la Ashkelon, yaligunduliwa mwaka 2013, lakini habari hizo zilifichuliwa Jumapili.
Habari
hizi ziliwekwa siri muda huo wote kuzuia kushambuliwa na waandamanaji
wa makundi ya Wayahudi wahafidhina ambao hawakutaka makaburi hayo
yafukuliwe. Mradi wa Leon Levy ulianzishwa miaka 30 iliyopita
Taarifa zinasema ugunduzi huo huenda ukafichua mengi
kuhusu asili ya Wafilisti ambao wamezungumziwa sana katika vitabu vya
kidini.
Mafanikio hayo yalitokea mwisho wa mwaka wa 30 wa uchimbaji ulioongozwa na kundi la Leon Levy Expedition.
Viongozi wa uchimbaji huo wanasema walipata makaburi yaliyozingirwa na manukato, vyakula, mapambo, vito na silaha.
Yanadaiwa kujengwa na kutumiwa kati ya karne ya 11 na karne ya 8 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu.
"Baada ya kutafiti kuhusu Wafilisti kwa miongo
mingi, hatimaye tunaweza kuwatazama,” anasema mmoja wa wanaakioloiia hao
Daniel M Master.
“Kwa ugunduzi huu, tunakaribia kubaini siri za asili yao.”
Wanaakiolojia hao sasa wanafanya uchunguzi wa DNA pamoja na uchunguzi wa miale ya ukaa kubaini watu hao waliishi wakati gani.
Profesa Lawrence E. Stager ni mmoja wa wanaoongoza utafiti huo
Watafiti hutofautiana kuhusu asili ya Wafilisti,
baadhi wakiamini walitoka Ugiriki, wengine visiwa vya Crete au Cyprus na
wengine eneo la Anatolia nchini Uturuki.
Wafilisti huoneshwa
katika Biblia kama maadui wakuu wa Waisraeli, na inadhaniwa walihamia
Israel kutoka maeneo ya Magharibi karne ya 12 kabla ya kuzaliwa kwa
Yesu.
Anayefahamika zaidi ni Goliath, mpiganaji ‘jitu’
ambaye kwa mujibu wa Biblia, aliuawa na Daudi kabla yake kuwa Mfalme wa
Waisraeli.
Katika Biblia, wanaoneshwa kama watu wakatili lakini
mabaki yaliyopatikana yanaonekana kuashiria kwamba walikuwa na ustaarabu
fulani.
TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.
SEHEMU YA PILI…. NASHIRIKI KUMFUNGA KICHAWI MUME WA MTU… . Katika makala yangu yaliyopita , nilieleza jinsi mungu wa k...
TAG SAYUNI OLDADAI
Karibu kwa huduma za kiroho pamoja na kumuabudu Mungu kwa pamoja aliye hai, katika kanisa la Tanzania Assemblies Of God, kanisa linalochungwa na mtumishi wa Mungu Meshack Mioki.
Not found any postsVIEW ALLReadmoreReplyCancel replyDeleteByHomePAGESPOSTSView All
USIPITWE NA HIZI HAPA CHINILABELARCHIVESEARCHALL POSTSNot found any post match with your requestBack HomeSundayMondayTuesdayWednesdayThursdayFridaySaturdaySunMonTueWedThuFriSatJanuaryFebruaryMarchAprilMayJuneJulyAugustSeptemberOctoberNovemberDecemberJanFebMarAprMayJunJulAugSepOctNovDecjust now1 minute ago$$1$$ minutes ago1 hour ago$$1$$ hours agoYesterday$$1$$ days ago$$1$$ weeks agomore than 5 weeks agoFollowersFollowTHIS CONTENT IS PREMIUMPlease share to unlockCopy All CodeSelect All CodeAll codes were copied to your clipboardCan not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy