http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Chadema Kanda ya Ziwa Watangaza Maandamano hadi Nyumbani kwa Rais Magufuli ( Chato )

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Ziwa kimetangaza kufanya maandamano katika kanda hiyo huku wakidai kuyafungia katik...


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Ziwa kimetangaza kufanya maandamano katika kanda hiyo huku wakidai kuyafungia katika mji wa Chato ambao ni nyumbani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Tamko la Chadema limetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho Kanda ya Ziwa Magharibi, Meshack Micus alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake.

“Sisi kama Chadema kanda ya Ziwa hasa kanda ya Victoria tayari tumeshawaelekeza wanachama wetu wote, viongozi wetu wote na tayari mwitikio ni mzuri. Na hadi leo tayari viongozi wetu wa vitongoji 1973 wameshajiandaa wako tayari kwa ajili ya kufanya maandamano na kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo yao,” alisema.

“Tutaandaa maandamano kutokea Kyelwa, tutaelekea Misenyo, Bukoba vijijini na tutakuja moja kwa moja mpaka Chato. Na wa Mwanza tayari nimeshawaagiza kwamba maandamano yetu tunaenda kuyafungia Chato,” aliongeza.

Tamko hilo limekuja ikiwa ni siku moja baada ya Rais John Magufuli kuwaonya Chadema kutomjaribu kwa kufanya maandamano bila kufuata utaratibu kwani hatawavumilia.

Rais Magufuli aliwataka wananchi kutokubali kudanganyika na kufanya maandamano na badala yake wajikite katika kufanya kazi itakayowaletea maendeleo.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kile walichokiita ‘Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (UKUTA)’, akiwaalika wafuasi wake kufanya maandamano nchi nzima kuanzia Septemba Mosi mwaka huu.

TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Chadema Kanda ya Ziwa Watangaza Maandamano hadi Nyumbani kwa Rais Magufuli ( Chato )
Chadema Kanda ya Ziwa Watangaza Maandamano hadi Nyumbani kwa Rais Magufuli ( Chato )
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiHZKJ3-Hjf2zNx6AQdbz5nwHe-32Oju0Bx19KZrCuSUcrMmAy2rD6HAbdlzQJcORMT4W9wX02ZlIYsZfjaMlFTyWUv-YQcIcc84UYTtX8QWVmgTAnlYVhhNersLukx95YB8KSyUbLAd-E/s1600/CHADEMA-LOGO.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiHZKJ3-Hjf2zNx6AQdbz5nwHe-32Oju0Bx19KZrCuSUcrMmAy2rD6HAbdlzQJcORMT4W9wX02ZlIYsZfjaMlFTyWUv-YQcIcc84UYTtX8QWVmgTAnlYVhhNersLukx95YB8KSyUbLAd-E/s72-c/CHADEMA-LOGO.png
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/07/chadema-kanda-ya-ziwa-watangaza.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/07/chadema-kanda-ya-ziwa-watangaza.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy