http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Wapinzani Waanika Sababu 6 za Kumng'oa Naibu Spika

Wabunge wa upinzani wameendelea kususia kwa siku ya tatu mfululizo vikao vya Bunge vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson tang...


Wabunge wa upinzani wameendelea kususia kwa siku ya tatu mfululizo vikao vya Bunge vinavyoendeshwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson tangu walipotangaza hatua hiyo Jumatatu wiki hii kwa kutokuwa na imani naye.

Tangu Jumanne wiki hii wabunge hao wamekuwa wakisusa vikao vinavyoongozwa na kiongozi huyo kwa madai kuwa anaminya demokrasia.

Siku hiyo wabunge hao waliingia bungeni kama kawaida na Dk Tulia alipomaliza tu kusoma dua ya kuliombea Bunge, walitoka hadi kipindi hicho kilipomalizika na naibu spika kumwachia mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kuongoza, ndipo wote waliporudi ukumbini na kuendelea na shu ghuli zao kama kawaida. 

Juzi, wabunge hao wote kama kawaida waliingia bungeni asubuhi na alipoingia Dk Tulia kuongoza kikao hicho, walisimama na kusikiliza dua ya kuliombea Bunge, kisha walitoka na kuwaacha wabunge wa CCM wakiendelea na Bunge.

Siku nzima ya juzi ambayo Dk Tulia aliendesha kikao cha asubuhi na jioni, wabunge hao hawakuhudhuria na ilipofika wakati wa kusoma hotuba ya msemaji wa kambi ya upinzani kwa Wizara ya Fedha na Mipango, David Silinde aliingia ukumbini akitokea nje na kuomba hotuba yake iingie kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge kama ilivyo. Kisha akasema: “Sitaisoma hapa kwa kuwa haturidhishwi na mwenendo wa Naibu Spika wa kutuendesha kama watoto.”

Wabunge hao wa upinzani walitoa sababu sita kwanini wanataka Dk Tulia aondolewe madarakani kwa Azimio la Bunge.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwa niaba ya wabunge hao, Mbunge wa Simanjiro, James Millya alizitaja sababu hizo kuwa ni kwanza Dk Tulia ameweka maslahi ya chama chake cha siasa mbele kuliko maslahi ya Bunge, kinyume na Kanuni ya 8(b) ya Bunge.

“Pili, Mei 6 alitumia vibaya madaraka ya kiti cha Spika kwa kutoa uamuzi wa mwongozo ambao ulikuwa unakiuka Ibara ya 12(2) ya Katiba. Muongozo huo uliokuwa unapinga udhalilishaji wa wabunge wanawake,” alisema.

Ya tatu ni kitendo cha Dk Tulia kuvunja Kanuni ya 64(1) (f) na (g) zinazokataza mbunge kutumia lugha ya matusi kwa mbunge mwingine ambapo alinukuliwa akisema “Mheshimiwa Bwege, usionyeshe ubwege wako humu ndani.” 

Alisema ya nne ni Mei 30 kiongozi huyo aliamua kwa makusudi kuvunja Ibara ya 63(2) ya Katiba na kutumia vibaya Kanuni ya 69(2) na 47(4) ya Kanuni za Bunge kumzuia Joshua Nassari kwa upande mmoja na Bunge zima kwa upande wa pili kutimiza majukumu yake ya kikatiba ya kusimamia na kuishauri Serikali.

“Sababu ya tano ni kuwa Mei 26, mwaka huu Dk Ackson akiongoza kikao cha Bunge bila ridhaa ya upinzani alishiriki kufuta sehemu ya hotuba ya msemaji wa upinzani kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kinyume cha kanuni ya 99(9) ya Bunge bila kushirikisha kamati yoyote ya Bunge,” alisema.

Sababu ya sita, Millya alisema kuwa ni kitendo cha Dk Ackson kukataa taarifa ya maoni tofauti, iliyowasilishwa na wabunge wanne wa upinzani.

TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Wapinzani Waanika Sababu 6 za Kumng'oa Naibu Spika
Wapinzani Waanika Sababu 6 za Kumng'oa Naibu Spika
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiqF_0QPqWhAl4aShFFBfVkxYtrROMDZmvqeKxMzaI1gfN9YIUclmd4e0OZecEC4S2LnjkpnP2L1Vxu0nENeO6p0LxyHZsCbUGwd5NTUR8WABAVF1IKdHUiRSzfnn7hLnjO1S9EonpyQk3F/s1600/1.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiqF_0QPqWhAl4aShFFBfVkxYtrROMDZmvqeKxMzaI1gfN9YIUclmd4e0OZecEC4S2LnjkpnP2L1Vxu0nENeO6p0LxyHZsCbUGwd5NTUR8WABAVF1IKdHUiRSzfnn7hLnjO1S9EonpyQk3F/s72-c/1.png
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/06/wapinzani-waanika-sababu-6-za-kumngoa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/06/wapinzani-waanika-sababu-6-za-kumngoa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy