http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Rais Magufuli Ahudhuria Ibada Kanisa La Mchungaji Antony Lusekelo, soma hapa alichonena...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitembelea Kanisa la Maombezi linaloongozwa na Mchungaji Antony Lusek...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitembelea Kanisa la Maombezi linaloongozwa na Mchungaji Antony Lusekelo (Mzee wa Upako) lililopo Ubungo Kibangu Jijini Dar es salaam na kuwaahidi waumini wa kanisa hilo kuwa Serikali yake itatengeneza barabara ya kutoka Ubungo Kibangu hadi River Side ambako itaungana na barabara ya Mandela.

Rais Magufuli ambaye amezungumza katika ibada ya asubuhi ya Kanisa hilo iliyofanyika leo tarehe 05 Juni, 2016 amesema amepita katika barabara hiyo ambayo imekuwa ikitumiwa na waumini wa kanisa hilo na wananchi wengine wa eneo la Ubungo Kibangu kwa lengo la kujionea hali halisi.

Aidha, Rais Magufuli amempongeza Kiongozi wa Kanisa hilo Mchungaji Antony Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako kwa huduma ya maombezi anayoitoa kwa waumini wake na watazamaji wanaofuatilia vipindi vyake vya Mahubiri kupitia Luninga.

“Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa mahubiri yako, kwa hiyo mahubiri unapoyatoa yanasambaa, kwa kweli mimi na familia yangu huwa yanatubariki sana, kwa hiyo nataka kukuthibitishia ninakupenda sana.

“Ndio maana kuna siku moja, ulizungumza kuhusu shida ya barabara yako ikabidi nitafute mbinu za namna gani tunaweza kuishughulikia kwa utaratibu ulio wazi, nikamtuma meneja wa barabara wa Mkoa wa Dar es salaam, akaja, akaipitia na akafahamu changamoto zilizopo, akafanya upembuzi yakinifu na usanifu, nataka kukuthibitishia kuwa fedha za kutengenezea barabara hii zipo” Amesema Dkt. Magufuli huku akishangiliwa na waumini.

Kwa upande wake Kiongozi wa Kanisa la Maombezi Mchungaji Antony Lusekelo (Mzee wa Upako) amemshukuru Rais Magufuli kwa kulitembelea kanisa hilo, na amemuombea heri katika uongozi wake ili aweze kufanikisha azma ya kuliletea taifa maendeleo ikiwemo mpango wa kuanzisha viwanda.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
05 Juni, 2016


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Rais Magufuli Ahudhuria Ibada Kanisa La Mchungaji Antony Lusekelo, soma hapa alichonena...
Rais Magufuli Ahudhuria Ibada Kanisa La Mchungaji Antony Lusekelo, soma hapa alichonena...
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEggp1A1okhO5jJGYJ0yym3qX7cYPPC8WraKgRyy7Uhtfo6lTDIDK5I22MHLzb5dVbYk7SfQbplQqFi63676XrwfAhjXoaKyaVJsyEQhNgD0KS_Xst3LAygcq-Ed78ZDpRDqS67pj-hKYTAH/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEggp1A1okhO5jJGYJ0yym3qX7cYPPC8WraKgRyy7Uhtfo6lTDIDK5I22MHLzb5dVbYk7SfQbplQqFi63676XrwfAhjXoaKyaVJsyEQhNgD0KS_Xst3LAygcq-Ed78ZDpRDqS67pj-hKYTAH/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/06/rais-magufuli-ahudhuria-ibada-kanisa-la.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/06/rais-magufuli-ahudhuria-ibada-kanisa-la.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy