watoto wa kanisa la TAG Sayuni Oldada katika picha ya pamoja wakiwa na mwalimu wao Magret Nnko. Watoto wa kikristo katika kanisa laTa...
![]() |
| watoto wa kanisa la TAG Sayuni Oldada katika picha ya pamoja wakiwa na mwalimu wao Magret Nnko. |
Sikuku hiyo ambayo huwa na lengo la watoto kuonyesha vipaji vyao, na kumpongeza mchungaji wa kanisa la mahali pamoja, wamempongeza mchungaji Meshack Mioki wa kanisa hilo kwa kumpatia zawadi mbali mbali.

Andiko kuu ya sikuku mwaka huu ni kutoka katika kitabu cha Marko 16; 15, ''Twendeni ulimwenguni tukahubiri injili kwa kila kiumbe'' Pamoja na kauli mbiu Watoto tuainuke tukawavune wenzetu.
Hataivyo mwalimu Adson Kagiye amefundisha somo lenye kichwa kisemayo, Mambo matano muhimu kwenye malezi ya watoto ili kuwahanda kufikia mafanikio yao.
jambo la kwanza ni kumpatia mtoto malezi Bora kwa kuonyesha upendo wa dhati kwake, Kumfundisha mtoto jinsi ya kuwajibika kuanzia akiwa mdogo,Kumpatia mtoto adhabu pale anapokosea,Kumfundisha kukosa na kupata pamoja na kupatia mtoto chakula bora.




