http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Kesi yavyama vya upinzani kuzuiliwa kila mara katika mikutano yao, latupliwa mbali na mahaka

KESI ya madai iliofunguliwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuiomba mahakama kup...


KESI ya madai iliofunguliwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuiomba mahakama kupiga marufuku zuio la Polisi, leo limetupiliwa mbali.
 
Mbowe alifungua kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2016, baada ya hivi karibuni Jeshi la Polisi  kupiga marufuku mikutano ya hadhara kwa madai kwamba, hali ya usalama nchini si salama.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, Kilimanjaro katika shauri hilo, aliwashtaki Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa madai wanahusika kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Mbowe ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, walitangaza kufanya oparesheni iliyopewa jina ‘Okoa Demokrasia nchini’ iliyokuwa na lengo la kuishtaki serikali kwa wananchi kwa kile alichodai, kuendesha nchi bila kufuata katiba ya nchi.

Hata hivyo, baada ya kupigwa marufuku kwa maandamano, Mbowe alifungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, akiiomba kutengua zuio hilo la polisi.

Mohammed Gwae, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, leo amepitia ombi lililopelekwa mahakamani hapo na upande wa mlalamikaji anayewakilishwa na mawakili John Mallya na Gasper Mwanalelya na kutoa uamzi.

Jaji Gwae akitoa uamuzi wa ombi la walalamikaji amedai kuwa, amefikia hatua hiyo baada ya walalamikaji kukosea kifungu cha kupeleka shauri hilo kortini kitendo kilichosababisha kulitupilia mbali.

Amesema kuwa, walalamikaji baada ya kupeleka ombi hilo kortini, upande wa wajibu maombi unaoongozwa na mawakili, Seth Mkemwa na Robert Kidando waliweka pingamizi wakiomba mahakama kutokusikiliza ombi hilo.

Jaji Gwae amesema kuwa, walalamikaji katika ombi lao walikosea kutumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha tatu cha sheria ya mwaka 2014 badala ya kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili ambacho kilitakiwa kutumiwa.

“Waleta maombi wametumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha tatu badala ya kutumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili kilichotakiwa kuwepo katika kuleta ombi na kama kifungu hiki hakijatumika hapo na ombi halipaswi kupokelewa,” amesema Jaji Gwae.

Hata hivyo Jaji Gwae amesema, licha ya kuwekewa pingamizi na wajibu maombi, walalamikaji wamesema kanuni na kifungu hicho ndivyo vilitakiwa kuwepo na hivyo vinavyopaswa kuwekwa sio sahihi.

Amesema kuwa, katika shauri la namna hiyo, kanuni na vifungu vilivyotakiwa kuwepo ni kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili na kanuni ya tano na kifungu kidogo cha sheria ya mwaka 2014 na kwamba wao waliviweka katika maelezo (Statements) badala ya (chember samers).

Mallya, mwanasheria wa mpeleka maombi amesema kuwa, baada ya kukosea kanuni na vifungu hivyo, watapeleka kwa mara nyingine ombi na kulifanyia marekebisho kama Jaji Mohamed Gwae alivyoelekeza.

TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Kesi yavyama vya upinzani kuzuiliwa kila mara katika mikutano yao, latupliwa mbali na mahaka
Kesi yavyama vya upinzani kuzuiliwa kila mara katika mikutano yao, latupliwa mbali na mahaka
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiovWADrFeGV6qG3bGFotxui3qib3QD2lC-aEzJ7c8WuvX354xCEy4luwfmpI8H7ke9oHmhfaObdmnqwpJwYXFdoIz_9k16EDB9LZpXGXNcjV0e4xgtJtbTmkiVZ26Ln6vnejtflwHdags6/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiovWADrFeGV6qG3bGFotxui3qib3QD2lC-aEzJ7c8WuvX354xCEy4luwfmpI8H7ke9oHmhfaObdmnqwpJwYXFdoIz_9k16EDB9LZpXGXNcjV0e4xgtJtbTmkiVZ26Ln6vnejtflwHdags6/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/06/kesi-yavyama-vya-upinzani-kuzuiliwa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/06/kesi-yavyama-vya-upinzani-kuzuiliwa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy