http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Alex Msama Amwangukia Mwakyembe Kumuomba Radhi Baada ya Gazeti la DIRA Analolimiliki Kuchapisha Habari Zenye Utata

Bw: Alex Msama, mmiliki wa gazeti la Dira . MFANYABIASHARA Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Sheria na Katiba,  Dk. Harrison Mwakyem...

Bw: Alex Msama, mmiliki wa gazeti la Dira.
MFANYABIASHARA Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Sheria na Katiba,  Dk. Harrison Mwakyembe kufuatia habari mbili zilizochapishwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania analolimiliki.
 
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msama alisema amejiridhisha kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari ‘Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa hadharani’ haikufuata misingi ya uandishi wa habari.

Habari nyingine ambayo imeonekana kumchafua Dk Mwakyembe ni ile ya Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2 ambazo zimemuumiza kiongozi huyo.

Alisema yeye kama mmiliki wa gazeti hilo amesikitishwa na habari hiyo na kwamba hatua ya kwanza anayoichukua ni kumuomba radhi Waziri Mwakyembe.

Msama alisema sambamba na kuomba radhi atamfikishia barua Mwakyembe ya kumtaka radhi kwa tukio hilo.

“Nimesikitishwa na habari hii kwa kuwa haikuzingatia misingi ya uandishi wa habari,  ilihukumu na kuonyesha kuwa lengo lake lilikuwa kumharibia jina Waziri Mwakyembe, ninachukua nafasi hii kumuomba radhi nikiwa mmiliki wa gazeti hilo,” alisema Msama.

Aidha Msama alisema hatua nyingine anayochukua ni kumsimamisha kazi mhariri wa gazeti hilo, Mussa Mkama kwa kuwa alishindwa kufanya kazi yake kwa umakini ya kuhakikisha habari anazozipitisha zinafuata misingi ya uandishi wa habari na weledi.

Alisema Mkama alipaswa kuhakikisha anafuata weledi lakini alishindwa kufanya hivyo kwa hiyo anamsimamisha kazi na kwamba hatua nyingine kali za kinidhamu zitafuata.

“Mimi ni mfanyabiashara sijui mambo ya uandishi, nilimuajiri nikiamini atasimamia yale aliyofundishwa chuoni, kwa kuwa ameshindwa inabidi akae pembeni kwanza,” alisisitiza Msama.

Ameahidi kuwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania litakalotoka Juni  27, kwa ukubwa uleule atamuomba radhi Waziri Mwakyembe.

Hivi karibuni  Waziri Mwakyembe aliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma akilalamikia kuwa habari mbili za gazeti hilo  iliyochapishwa na Gazeti la Dira ya Mtanzania la Juni 20 na la Juni 23 mwaka huu zililenga kumchafua na kuahidi kuwa atalishtaki kupitia habari hizo mbili.

TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Alex Msama Amwangukia Mwakyembe Kumuomba Radhi Baada ya Gazeti la DIRA Analolimiliki Kuchapisha Habari Zenye Utata
Alex Msama Amwangukia Mwakyembe Kumuomba Radhi Baada ya Gazeti la DIRA Analolimiliki Kuchapisha Habari Zenye Utata
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhBXmhVu7YIZHVH5qF3K7FBXelUg3qbY2WYS2U3V0z0tblKRo59lS-rvhLEw8ntYGRnLg_giJc6QRQCp0V6BdfbNQMAEUyg-Pe0CK7rjVAJVe31erXMhc6Pw4ZnJD0Q2VA17ywqJ8cM2e0/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhBXmhVu7YIZHVH5qF3K7FBXelUg3qbY2WYS2U3V0z0tblKRo59lS-rvhLEw8ntYGRnLg_giJc6QRQCp0V6BdfbNQMAEUyg-Pe0CK7rjVAJVe31erXMhc6Pw4ZnJD0Q2VA17ywqJ8cM2e0/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/06/alex-msama-amwangukia-mwakyembe_46.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/06/alex-msama-amwangukia-mwakyembe_46.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy