Ugaidi: Shambulizi la kimeta latibuka Kenya Mohammed Abdi Ali -amekamatwa Polisi nchini Kenya wamemkamata mtu mmoja ...
Ugaidi: Shambulizi la kimeta latibuka Kenya
| Mohammed Abdi Ali -amekamatwa |
Polisi nchini Kenya
wamemkamata mtu mmoja wanayesema alikuwa kiongozi wa genge la madaktari
watatu waliokuwa wakipanga njama ya kutekeleza shambulizi la kigaidi
linalofanana na lile lililotekelezwa Septemba mwaka wa 2014 kwenye
maduka ya jumla ya Westgate mjini Nairobi.
Mohammed Abdi Ali anayejifunza kuwa daktari katika hospitali moja anadaiwa kuwa ni kiongozi wa kundi hilo la watatu ambao lilikuwa linapanga mashambulizi hayo.
| Ahmed Hish-mshukiwa |
Ali anadaiwa kuwa mwanachama wa kundi la Islamic State.
| Farah Dagane-mshukiwa |
Polisi hata hivyo wametoa majina yao na kuchapisha picha za Ahmed Hish na Farah Dagane, ambao sawa na Ali wanajifunza kuwa madaktari.



