http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Mwanafunzi Mbaroni Kwa Kumtukana Rais Pamoja Na Mkuu Wa Majeshi Mwamunyage.

Jeshi la polisi mkoani Arusha linamshikilia mwanafunzi wa Mwaka wa tatu wa chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru aliy...

SeeBait


Jeshi la polisi mkoani Arusha linamshikilia mwanafunzi wa Mwaka wa tatu wa chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru aliyejulikana kwa jina la Harold Mmbando (23) mkazi wa Arusha kwa kosa la kutoa taarifa za uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu wa majeshi Davis Mwamunyange pamoja na kusambaza ujumbe wa maneno makali juu ya viongozi hao.

Akiongelea tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa tukio hilo lilitokea May 17 mwaka huu majira ya saa 09:00 asubuhi .

Alisema kuwa mwanafunzi huyo alitoa taarifa za uchochezi kuhusu mkuu wa majeshi ambapo alimtaka mkuu huyo wa majeshi kupindua nchi na kusema kuwa haiwezekani viongozi wote wawe nje ya nchi huku akuna kiongozi aliyepewa mamlaka ya kukikaimu kiti.

Mtuhumiwa huyo aliandika maneno haya ,Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti,hayo ndio maneno aliyoyasema mtumiwa huyo “alisema Mkumbo.

Aidha aliongeza kuwa mbali na maneno hayo pia mtumiwa huyo alisambaza ujumbe mwingine wenye maneno yafuatayo,Dr Shein akiuawa kama Karume sitashangaa wala kustuka naomba mungu mauaji ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwa viongozi wa kisasa hasa watawala na sio wananchi wa kawaida hayo ndio maneno aliyoyaandika mtuhumiwa huyo kupitia mitandao ya kijamii kama facebook."

Mkumbo alisema kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi tu upelelezi utakapo kamilika,huku akitoa rai kwa watu wote wanaotumia mitandao ya kijamii kutumia mitandao hiyo ya kijamii pasipo kukiuka sheria na taratiu za kisheria .

Alitumia muda huo pia kutoa onyo kali kwa yoyote atakaye bainika anatumia mitandao vibaya na kusema kuwa atachukuliwa hatua kali za kisheria dhidi yake.
 
Wakati hayo yakiendelea mshtakiwa wa kesi ya kumtukana Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Isaac Emily (40), mkazi wa Olasiti jiji hapa inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Juni 5 mwaka huu katika mahakama ya hakiku mkazi Arusha

CHANZO......MPEKUZI

TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mwanafunzi Mbaroni Kwa Kumtukana Rais Pamoja Na Mkuu Wa Majeshi Mwamunyage.
Mwanafunzi Mbaroni Kwa Kumtukana Rais Pamoja Na Mkuu Wa Majeshi Mwamunyage.
http://seebait.com/assets/images/favicon.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEinlemnLbHsaXz9ytVoEtQjC8PFdV600AyPbQHSPa9roEANVQiDu60T4utciIPtGcyp_Mpo3jYawomZHf9oabMfxD6vtOOveNXXlHH9I3RdYqNb0C-XNisMl0kIb2mJuFjfrVALn-mpbN4F/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/05/mwanafunzi-mbaroni-kwa-kumtukana-rais.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/05/mwanafunzi-mbaroni-kwa-kumtukana-rais.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy