http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Mkuu wa Mkoa Afumaniwa Akifanya Mapenzi na Mwanae

Mkuu wa zamani wa Mkoa wa Kaskazini Pemba na mshauri wa Rais wa Zanzibar kisiwani humo, Dadi Faki Dadi amekamatwa akituhumiwa kufanya m...


Mkuu wa zamani wa Mkoa wa Kaskazini Pemba na mshauri wa Rais wa Zanzibar kisiwani humo, Dadi Faki Dadi amekamatwa akituhumiwa kufanya mapenzi na mtoto wake wa kambo.

Dadi alikamatwa juzi akidaiwa kukutwa na mtoto huyo wa mkewe wa ndoa mwenye umri wa miaka 21 katika nyumba ya kulala wageni inayoitwa Executive, jirani na makao makuu ya Uhamiaji Zanzibar katika eneo la Kilimani chini na Maisara, mjini Unguja.

Mwanasiasa huyo alijikuta akipigwa pingu na polisi akiwa kifua wazi mbele ya mkewe na wanafamilia na kisha kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Mwembemadema.

Picha za video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zilimwonyesha Dadi akikabiliwa na mashambulizi makali ya maneno kutoka kwa watu waliomkamata, akiwamo mkewe.

“Mwacheni avae nguo kwanza, mpeleke bwana, twende bwana..." ni baadhi ya maneno yanayosikika katika video iliyorekodiwa wakati wa kumtia mbaroni.

Taarifa zilizopatikana miongoni mwa wanafamilia ya kiongozi huyo, zilidai kwamba alikamatwa baada ya kumtilia shaka binti huyo kutokana na mienendo yake ya hivi karibuni na kuamua kumfuatilia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alithibitisha kumshikilia Dadi kwa muda kabla ya kumwachia kwa dhamana.

“Kijamii alitenda kosa, lakini sisi tunaendelea kufanya uchunguzi, iwapo tutabaini ametenda kosa la kisheria na anaweza kuwa mashtaka tutamkamata ili kumpeleka katika vyombo vya sheria,” alisema Mkadam.

Mmoja wa wanafamilia ambaye aliomba jina lake lisitajwe alisema:“Mwizi siku zake ni arobaini, tulimtega na hatimaye tumemnasa sasa tuone mwisho wake utakuwa nini na kipi kitajiri baadaye.”

TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mkuu wa Mkoa Afumaniwa Akifanya Mapenzi na Mwanae
Mkuu wa Mkoa Afumaniwa Akifanya Mapenzi na Mwanae
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhg9dIaaBTmPWHNgANZW47ITTEgpqTtSLNibG1_P2pBeHaUErqf77xIwFTYkT1MGVektuOoHIVeCMKwH9fPnl2yrWMKNLDs09ytQCodK4VXMAV5xLuYB-9sNOaieGy8O4Xo-nDh_xDxY1qF/s1600/3.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhg9dIaaBTmPWHNgANZW47ITTEgpqTtSLNibG1_P2pBeHaUErqf77xIwFTYkT1MGVektuOoHIVeCMKwH9fPnl2yrWMKNLDs09ytQCodK4VXMAV5xLuYB-9sNOaieGy8O4Xo-nDh_xDxY1qF/s72-c/3.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/05/mkuu-wa-mkoa-afumaniwa-akifanya-mapenzi.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/05/mkuu-wa-mkoa-afumaniwa-akifanya-mapenzi.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy