http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

DIWANI MBARONI KWA KUBAKA

Diwani wa Mtibwa wilayani Mvomero, Lucas Edward (38) maarufu Mwakambaya anashikiliwa na Polisi Mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kumbaka bin...

Diwani wa Mtibwa wilayani Mvomero, Lucas Edward (38) maarufu Mwakambaya anashikiliwa na Polisi Mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 14, mkazi wa Turiani kwenye nyumba ya kulala wageni.

Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Ulrich Matei alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Mei 29 saa 12 jioni kwenye nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Sultan, Manispaa ya Morogoro.

Matei alisema polisi walipata taarifa kutoka kwa msiri wao kwamba katika nyumba hiyo, kuna mtu ameonekana akiwa na binti mdogo, hivyo askari walifuatilia nyendo zake na kumkamata.

Alisema askari baada ya kufika kwenye nyumba hiyo, walimkuta mtuhumiwa huyo akiwa na binti huyo chumba namba 108.

Alisema uchunguzi wa kitabibu unaendelea kuthibitisha tuhuma hizo.

Akizungumza kwa simu, Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Mvomero, Mrisho Ramadhan alithibitisha kukamatwa kwa diwani huyo na kwamba mpaka sasa hajafahamu ni kwa tuhuma gani.

Ramadhan alisema kwa sasa wao kama viongozi wa chama wanafuatilia kujua tuhuma na ameomba uongozi wa Chadema Mkoa kufuatilia zaidi na kwamba, atatoa taarifa baada ya kufahamu kwa undani.

“Ni kweli nimesikia mheshimiwa kakamatwa huko mjini Morogoro, sijajua kosa nimewaomba viongozi wa Mkoa Chadema kufuatilia nitatoa maelezo baadaye,” alisema Ramadhan.

Alisema baada ya kupata undani wa tukio hilo, atatoa taarifa ili kujulisha umma kilichotokea.


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : DIWANI MBARONI KWA KUBAKA
DIWANI MBARONI KWA KUBAKA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiwh5U5PVgX02_rbJdRo5vhYJyMewd3QnkkHPyBdUai1cxwoEPNs4F68eXHAvGq14J-UtG6AS8xH2hZ2BDKuliZYeUnVlwoplKYDswHN9hi0hCO3IKmyhyphenhyphenAun7_yYOGUyjfnnU_qAPU9n9o/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiwh5U5PVgX02_rbJdRo5vhYJyMewd3QnkkHPyBdUai1cxwoEPNs4F68eXHAvGq14J-UtG6AS8xH2hZ2BDKuliZYeUnVlwoplKYDswHN9hi0hCO3IKmyhyphenhyphenAun7_yYOGUyjfnnU_qAPU9n9o/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/05/diwani-mbaroni-kwa-kubaka.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/05/diwani-mbaroni-kwa-kubaka.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy