Dkt Riek Machar anatarajiwa kutawazwa kuwa makamu wa rais kulingana na mkataba wa amani Waasi nchini Sudan Kusini wanasema kuwa wanach...
![]() |
| Dkt Riek Machar anatarajiwa kutawazwa kuwa makamu wa rais kulingana na mkataba wa amani |
Waasi nchini Sudan Kusini wanasema
kuwa wanachama wake 16 wa kitengo cha habari, wamekamatwa na kupigwa
vibaya na maafisa wa usalama katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba.
Dkt Riek Machar anatarajiwa kutawazwa kuwa makamu wa rais kulingana na mkataba wa amani uliositisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyoanza Desemba mwaka wa 2013 kati ya waasi wanaomuunga mkono bw Machar na wanajeshi watiifu kwa rais Salva Kiir.
Walikuwa wakijaribu kuwakusanya watu ili kumkaribisha naibu mwenyekiti vuguvugu la waasi, Alfred Ladu Gore.
Walitakiwa kuhakikisha kuwa usalama wa Bwana Machar, ambaye aliteuliwa majuzi kuwa makamu wa Rais, uko sawa.





