Furaha ya ushindi mjini New York Zaidi ya nusu ya kura zilizohesabiwa katika uchaguzi wa awali wa urais nchini mareka...
| Furaha ya ushindi mjini New York |
Zaidi ya nusu ya kura zilizohesabiwa
katika uchaguzi wa awali wa urais nchini marekani katika mji wa New
york,zinaonesha kwamba Donald Trump na Hillary Clinton wamepata ushindi
mkubwa Zaidi ndani ya vyama vyote viwili.
Hata hivyo New York inatajwa kuwa ngome nyingine ya Donald Trump,ambapo Cruz yeye hesabu za kura zake zimeonekana kugoma mapema kabisa katika chama chake cha Repubilcan .
Wakati Hillary Clinton amemshinda mpinzani wake Bernie Sanders kwa ushindi mkubwa .Hillary amewaambia wapinzani wake kuwa kuna la ziada linalowafanya wawe wamoja Zaidi ya kuwagawa.



