http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

TAASISI YA WANAUME JIJINI ARUSHA YALAANIVITENDO VYA USHOGA

Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanaume Man at Work Maxwell Stansalaus akizungumza na Wanaume jana jijini Arusha katika...

ANDREA NGOBOLE



Mwanzilishi wa Taasisi ya Wanaume Man at Work Maxwell Stansalaus akizungumza na Wanaume jana jijini Arusha katika mkutano Mkuu wa Wanaume uliofanyika jana na kuhudhuriwa na zaidi ya wanaume 700 ambao lengo lake ni kuwakumbusha wanaume wajibu walionao kwa familia,jamii na taifa.Picha na Ferdinand Shayo





Na Ferdinand Shayo,Arusha.


Taasisi isiyo ya  kiserikali ya Wanaume Kazini maarufu kama Man at Work imelaani vikali vitendo vya ushoga vinavyoshusha hadhi na thamani ya wanaume hivyo wameitaka serikali kupiga vite vitendo hivyo ambavyo ni kunyume cha Maadili ya Tanzania na Afrika kwa Ujumla.

Muasisi wa Taasisi hiyo  yenye makao yake jijini Arusha Maxwell  Stanslaus  amesema kuwa Wanaume kazini wanapinga vikali vitendo vya ushoga kwa zaidi ya Asilimia 100% na kuwataka wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha Mara moja.

Maxwell alisema hayo jana katika mkutano Mkuu wa Wanaume kazini uliofanyika jijini hapa huku akisema kuwa taasisi hiyo imelenga kuhimiza wanaume kote nchini kutimiza wajibu wao na kutenda majukumu yao kama wanaume katinga ngazi ya familia,jamii na taifa ili kuchochea maendeleo.

“Kwa sasa tunaona nidhamu ya serikali imerudi kutokana na Mwanaume mmoja tu Rais John Pombe Magufuli kuamua kutimiza wajibu yake hivyo Basi  Wanaume zaidi ya Milioni  walioko Tanzania wakiamua kutimiza majukumu yao na wajibu Tanzania itanyooka” Alisema  Maxwell

Moja kati ya Wanaume waliohudhuria ni Joseph Mayagila alisema kuwa matatizo ya ushoga yanatokana na baadhi ya wanaume kujisahau na kujaribu kuwa wanawake ,jukwaa hili la wanaume ni muhimu kuwakumbusha wanaume juu ya uanaume wao na kutimiza yale yanayowapasa kama wanaume.

Dokta Emmanuel Buganga  ameeleza kuwa vuguvugu la wanawake kudai haki zao linatokana na baadhi ya wanaume kutotimiza wajibu wao kama wanaume wameacha majukumu yao ya kutunza familia zao na kuwa walezi na walinzi wa familia .


Mhamasishaji wa Masuala ya kijamii Samuel Sasali amesema kuwa wanaume wengi wamejisahau sana katika masuala ya malezi ya familia kwani usimpolea mtoto katika njia impasayo atakuja kukuaibisha ukubwani

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : TAASISI YA WANAUME JIJINI ARUSHA YALAANIVITENDO VYA USHOGA
TAASISI YA WANAUME JIJINI ARUSHA YALAANIVITENDO VYA USHOGA
http://lh5.googleusercontent.com/-Dr-SnIEnan4/AAAAAAAAAAI/AAAAAAAABqE/HG6Jw5Md2wo/s512-c/photo.jpg
http://lh5.googleusercontent.com/-Dr-SnIEnan4/AAAAAAAAAAI/AAAAAAAABqE/HG6Jw5Md2wo/s72-c/photo.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/04/taasisi-ya-wanaume-jijini-arusha.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/04/taasisi-ya-wanaume-jijini-arusha.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy